TABORA United yasalia Ligi Kuu ya NBC 2024/2025
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA
TABORA United yasalia Ligi Kuu ya NBC 2024/2025
TABORA United yasalia Ligi Kuu ya NBC 2024/2025, Klabu ya Tabora United imefanikiwa kusalia Ligi Kuu ya NBC kwa msimu ujao wa 2024/2025 baada ya kuibuka na Ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Biashara United hivyo Kuvuka hatua hiyo ya mtoano kwa ushindi wa jumla 2-1.
Ikumbukwe kwenye mchezo wa kwanza uliochezwa mkoani Mara kwenye uwanja wa Karume Juni 12-12024, Biashara United iliibuka na ushindi wa bao 1-0.
Kabla ya kukutana na Biashara Tabora United iliianza hatua hii ya mtoano kwa kucheza na JKT Tanzania na kupoteza kwa jumla ya mabao 4-0 huku Biashara United wakishinda kwa jumla ya mabao 4-0 dhidi ya Mbeya Kwanza.
Sasa rasmi Tabora United itashiriki Ligi Kuu ya NBC huku Biashara United ikisalia Ligi ya NBC Championship msimu wa 2024/2025.