RATIBA YA LIGI KUU YA NBC 2024/2025 TAZAMA HAPA


INEC RATIBA YA UBORESHAJI WAPIGA KURA 2024/2025 HAPA


INEC KUITWA KWENYE USAILI 2024/2025 TAZAMA HAPA


AJIRA MPYA KILA SIKU TAFADHALI BONYEZA HAPA


JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP HAPA


TANGAZO la Wito kwa Wahitimu wa Kada ya Famasi Kutambuliwa

Filed in Ajira by on 03/08/2024
SHARE THIS POST:

JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA

TANGAZO la Wito kwa Wahitimu wa Kada ya Famasi Kutambuliwa

TANGAZO la Wito kwa Wahitimu wa Kada ya Famasi Kutambuliwa

TANGAZO la Wito kwa Wahitimu wa Kada ya Famasi Kutambuliwa

TANGAZO la Wito kwa Wahitimu wa Kada ya Famasi Kutambuliwa,Baraza la Famasi limeanzishwa chini ya Kifungu Na. 3 cha Sheria ya Famasi, Sura 311 kwa lengo la kusimamia taaluma ya famasi nchini.

Pamoja na majukumu mengine, Kifungu Na. 4 cha Sheria kinaelekeza Baraza kusajili, kuandikisha na kuorodhesha wafamasia, fundi dawa sanifu, na fundi dawa wasaidizi wenye sifa na weledi ili kutoa huduma za kitaaluma.

Aidha, Kifungu Na.24(1) na 28(1) kinaeleza kuwa mtu yeyote hataruhusiwa kutoa huduma za dawa kama fundi dawa sanifu na fundi dawa msaidizi bila kuandikishwa au kuorodheshwa chini ya sheria hiyo.

Hivyo basi, Ofisi ya Msajili inatoa wito kwa wahitimu wote wa kada ya famasi kwa ngazi ya stashahada na astashahada waliohitimu kabla ya Mwaka 2016 ambao bado hawajaandikishwa au hawajaorodheshwa kufika katika Ofisi ya Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri zilizopo karibu wakiwa na nyaraka zifuatazo kwaajili ya kutambuliwa:

  • Cheti cha kuhitimu masomo (Darasa la Saba au Kidato cha nne au sita);
  • Cheti cha kuhitimu masomo ya stashahada au astashahada; c) Kitambulisho cha Taifa (NIDA) au Mpiga Kura au Udereva; na d) Maelezo binafsi (CV) yasiyozidi ukurasa mmoja (01).

Zoezi la utambuzi limeanza tarehe 29 Julai hadi 16 Agosti, 2024.

Endapo utahitaji msaada zaidi tafadhali wasiliana Baraza la Famasi Tanzania kupitia simu bila malipo namba 0800110015 au namba 0736222503/0736222516.
Imetolewa Na; Msajili,
Baraza la Famasi
S.L.P. 1277, Dodoma
info@pc.go.tz

PATA NYIMBO ZOTE MPYA BONYEZA HAPA

MATANGAZO YA BIASHARA WASILIANA NASI KUPITIA nijuzehabariblog@gmail.com

SHARE THIS POST:

Tags:

Comments are closed.