RATIBA YA LIGI KUU YA NBC 2024/2025 TAZAMA HAPA


INEC RATIBA YA UBORESHAJI WAPIGA KURA 2024/2025 HAPA


INEC KUITWA KWENYE USAILI 2024/2025 TAZAMA HAPA


AJIRA MPYA KILA SIKU TAFADHALI BONYEZA HAPA


JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP HAPA


TANZIA Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi Afariki Dunia

Filed in Habari, Michezo by on 29/02/2024
SHARE THIS POST:

JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA

TANZIA Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi Afariki Dunia

TANZIA: Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi Afariki Dunia, Slogan of Ali Hassan Mwinyi,Watoto wa mzee ali hassan mwinyi,Ali hassan mwinyi afariki, Alli Hassan Mwinyi Afariki Dunia.

TANZIA: Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi Afariki Dunia

TANZIA Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi Afariki Dunia, Slogan of Ali Hassan Mwinyi,Watoto wa mzee ali hassan mwinyi,Ali hassan mwinyi afariki, Alli Hassan Mwinyi Afariki Dunia.

Rais wa awamu ya pili wa Tanzania, Ali Hassan Mwinyi amefariki dunia leo Alhamisi, Februari 29, 2024 katika Hospitali ya Mzena, Kijitonyama jijini Dar es Salaam alipokuwa akipatiwa matibabu.

Rais wa zamani wa Tanzania Ali Hassan Mwinyi amefariki Dunia leo Alhamisi, Februari 29, 2024 katika Hospitali ya Mzena, Kijitonyama jijini Dar es Salaam alipokuwa akipatiwa matibabu akiwa na umri wa miaka 98, Rais Samia Suluhu Hassan ametangaza.

TANZIA Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi Afariki Dunia

TANZIA: Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi Afariki Dunia, Slogan of Ali Hassan Mwinyi,Watoto wa mzee ali hassan mwinyi,Ali hassan mwinyi afariki, Alli Hassan Mwinyi Afariki Dunia.Mwinyi alikuwa Rais wa pili wa Tanzania kuanzia 1985-1995 akimrithi Rais mwanzilishi Julius Kambarage Nyerere.

Mzee Mwinyi amefariki Dunia saa 11 jioni ya leo Alhamisi Februari 29,2024 katika Hospitali ya Mzena, Kijitonyama jijini Dar es Salaam.

“Kwa majonzi makubwa nasikitika kutangaza kifo cha Rais mstaafu wa Tanzania, Ali Hassan Mwinyi, aliyefariki dunia leo Februari 29 saa 11 jioni katika Hospitali ya Mzena Jijini Dar es Salaam alipokuwa akipatiwa matibabu ya saratani ya mapafu.

Mwinyi amefariki miezi mitatu kabla ya kutimiza miaka 99.

Historia ya Ali Hassan Mwinyi

Ali Hassan Mwinyi (8 Mei 1925 – 29 February 2024) alikuwa Rais wa pili wa Tanzania kuanzia mwaka 1985 hadi 1995. Aliyemtangulia ni Mwalimu Julius Nyerere, na aliyemfuata ni Benjamin Mkapa. Pia alikuwa mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuanzia mwaka 1990 hadi 1996.

Ali Hassan Mwinyi


Rais wa Tanzania
Muda wa Utawala
5 November 1985 – 23 November 1995
Waziri Mkuu Joseph Sinde Warioba
mtangulizi Julius Nyerere
aliyemfuata Benjamin Mkapa

tarehe ya kuzaliwa 8 Mei 1925 (umri 98)
Tanganyika
utaifa Mtanzania
chama CCM
ndoa Siti Mwinyi
dini Uislamu

Kabla ya hapo alikuwa Rais wa tatu wa Zanzibar baada ya kujiuzulu kwa mtangulizi wake Aboud Jumbe Mwinyi kwenye Januari 1984.

Urais wa Zanzibar ulimfanya kuwa makamu wa rais wa Tanzania; hivyo aliteuliwa kugombea urais wa kitaifa wakati Julius Nyerere alipoamua kutogombea tena kwenye mwaka 1985.

Mwinyi alichaguliwa akaacha cheo chake cha Zanzibar akawa rais wa Tanzania. Visiwani alifuatwa na Idris Abdul Wakil.

Kabla hajachaguliwa kuwa Rais, Mwinyi alikuwa Waziri wa Mambo ya Ndani na Makamu Rais.

Maisha
Mwinyi alizaliwa Kivure kwenye Mkoa wa Pwani wa Tanzania bara lakini wazazi wake walihamia Unguja alipokuwa mdogo. Kuanzia mwaka 1933 alipokea elimu ya msingi na sekondari kwenye shule za Mangapwani na Dole Secondary School alikohitimu mwaka 1942. Baada ya masomo ya ualimu aliendelea kwenye Chuo Kikuu cha Durham nchini Uingereza.

Alianza kufundisha shuleni akaendelea kuwa mkuu wa chuo cha ualimu Unguja hadi kuteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa wizara ya elimu ya Zanzibar baada ya mapinduzi kwenye mwaka 1963.

Mnamo 1970 alipewa uwaziri wa nchi katika ofisi ya rais akaendelea na vyeo mbalimbali katika serikali ya Zanzibar, pamoja na waziri wa afya, wa mambo ya ndani na wa utalii.

Alihudumia pia miaka mitano kama balozi wa Tanzania nchini Misri. Kwenye Januari 1984 aliteuliwa kuwa rais wa Zanzibar baada ya mtangulizi wake Aboud Jumbe Mwinyi alilazimishwa kujiuzulu.

Katika nafasi kama rais wa Zanzibar alikuwa pia makamu wa rais wa maungano; katika uchaguzi wa 1985 aliteuliwa na CCM kuwa mgombea kwa nafasi ya raisi wa taifa akachaguliwa bila mpinzani katika mfumo wa chama kimoja.

Wakati wa urais wa kitaifa wa Mwinyi, sera za Ujamaa zilianza kugeuzwa. Badala yake sera za soko huria zilianzishwa, masharti ya kuingiza bidhaa kutoka nchi za nje yalipunguzwa na uanzishaji wa biashara ya watu binafsi ulihamasishwa.

Mwaka wa 1991, Mwinyi alianzisha Tume ya Nyalali iliyopendekeza kuanzisha mfumo wa vyama vingi nchini. Wakati wa awamu yake kwenye mwaka 1995 ulitokea uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi vya kisiasa nchini Tanzania.

Sera za soko huria za Mwinyi zimeendelezwa chini ya Rais Benjamin Mkapa. Mwinyi mwenyewe, baada ya kustaafu, hakujiingiza katika mambo ya siasa tena. Anaendelea kuishi huko Dar es Salaam.

Gazeti la Mfanyakazi la wakati huo—liliripoti habari ya ushindi wa Ali Hassan Mwinyi kwa kupata kura kwa kishindo.

Heshima na Tuzo

Nishani

Nishani Nchi Mwaka Ref
Nishani ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Bendera ya Tanzania Tanzania 2011

Shahada za Heshima

Chuo Kikuu Nchi Shahada ya Uzamivu Mwaka Ref
Chuo Kikuu Huria cha Tanzania Bendera ya Tanzania Tanzania Daktari wa Barua 2012 [3]
Chuo Kikuu cha Afrika Mashariki Bendera ya Kenya Kenya Daktari wa Usimamizi wa Biashara 2013

PIA UNAWEZA KUSOMA👇

PATA NYIMBO ZOTE MPYA BONYEZA HAPA

MATANGAZO YA BIASHARA WASILIANA NASI KUPITIA nijuzehabariblog@gmail.com

SHARE THIS POST:

Tags: , , , ,

Comments are closed.