TAUSI hatua za Kufuata ili Upate Leseni
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA
TAUSI hatua za Kufuata ili Upate Leseni
TAUSI hatua za Kufuata ili Upate Leseni, Hatua za Kufuata Upate Leseni Mfumo Wa TAUSI,Mfumo TAUSI utasaidia kupunguza muda na kuondoa urasimu uliokuwepo kwa baadhi ya sehemu.
Na sehemu nyingine ambayo kulikuwa na taarifa za rushwa, mfumo huu umepunguza adha hizo kwa sababu Afisa Biashara hakutani moja kwa moja na mwananchi.
Hatua za Kufuata Ili Upate Leseni ya Biashara kwenye Mfumo Wa TAUSI.
Mahitaji wakati wa Usajili.
- Namba ya NIDA
- Namba ya Simu iliyosajiliwa Kwa namba ya NIDA yako.
- Barua pepe (Email)
Mahitaji ya Maombi ya Leseni (Maombi binafsi)
- TIN Number
- Mkataba wa Pango (Hati ya kupangisha eneo ilipo biashara yako)
- Tax Crearance (Hati inayotolewa na TRA)
Mahitaji ya Maombi ya Leseni (Maombi Kwa wenye Kampuni)
- TIN Number
- Mkataba wa Pango (Hati ya kupangisha eneo ilipo biashara yako)
- Tax Crearance (Hati inayotolewa na TRA)
- TIN Number ya Mwakilishi wa Kampuni
- Memorandum
- Certificate of incorporation
- Namba ya NIDA ya Mwakilishi wa Kampuni
Baada ya kukamilisha mahitaji hayo sasa unaweza kuomba leseni ya biashara, vileo na kulipia ada ya matumizi ya choo, ushuru wa kushusha na kupakia, ushuru wa Samaki na mazao yake kwa njia ya mtandao kupitia Mfumo wa TAUSI kwa kubonyeza TAUSI MAOMBI YA LESENI.