TFF Yafanya Mabadiliko Utolewaji wa Tuzo za Ligi Kuu
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA
TFF Yafanya Mabadiliko Utolewaji wa Tuzo za Ligi Kuu
TFF Yafanya Mabadiliko Utolewaji wa Tuzo za Ligi Kuu,Tuzo za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) sasa zitakuwa zikifanyika wakati wa michezo ya Ngao ya Jamii.
Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Afisa Habari na Mawasiliano wa TFF, Cliford Ndimbo imeeleeza kuwa lengo la mabadiliko ya hafla hizo za kuwatuza Wachezaji Bora, ni kufanya Maboresho ya kulifanya tukio hilo kuwa bora zaidi kukidhi malengo na mahitaji yake.
Kwa mabadiliko hayo, hafla ya tuzo za TFF kwa msimu wa 2023/2024 itafanyika wakati wa mchezo wa Ngao ya Jamii kufungua msimu wa 2024/2025.
Tuzo za TFF ni tukio la kuwazawadia wanamichezo waliofanya vizuri katika mashindano yanayoandaliwa na TFF kupitia Bodi ya Ligi (TPLB) na matukio mengine rasmi yenye kuambatana na mpira wa miguu hapa nchini.