RATIBA YA LIGI KUU YA NBC 2024/2025 TAZAMA HAPA


INEC RATIBA YA UBORESHAJI WAPIGA KURA 2024/2025 HAPA


INEC KUITWA KWENYE USAILI 2024/2025 TAZAMA HAPA


AJIRA MPYA KILA SIKU TAFADHALI BONYEZA HAPA


JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP HAPA


TPLB Yaondoa Dakika za Nyongeza Ngao ya Jamii 2024

Filed in Michezo by on 24/07/2024
SHARE THIS POST:

JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA

TPLB Yaondoa Dakika za Nyongeza Ngao ya Jamii 2024

TPLB Yaondoa Dakika za Nyongeza Ngao ya Jamii 2024

TPLB Yaondoa Dakika za Nyongeza Ngao ya Jamii 2024

TPLB Yaondoa Dakika za Nyongeza Ngao ya Jamii 2024,Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara (TPLB), imebainisha kuwa hakutokuwa na dakika za nyongeza kwa Michezo yote itakayopigwa kwenye Ngao ya Jamii inayotarajiwa kuanza Agosti 8,2024.

Ofisa Habari wa Bodi hiyo, Karim Boimanda, amesema kuwa mechi zote zitachezwa kwa dakika 90 na baada ya hapo ni mikwaju ya penalti itaamua mshindi.

Boimanda alisema hayo, alipokuwa akibainisha baadhi ya kanuni zitakazotumika kwenye michuano hiyo, pamoja na Ligi Kuu Tanzania Bara inayotarajiwa kuanza Agosti 16, mwaka huu

Mbali na hayo, amesema wachezaji watakaotumika kwenye mechi hizo ni wale tu ambayo watakuwa wamekamilisha usajili wa kucheza Ligi Kuu na si vinginevyo kwani huko nyuma imeshawahi kutokea timu moja kuchezesha kwenye Ngao ya Jamii mchezaji ambaye baadaye ilibainika bado alikuwa hajakamilisha taratibu za kucheza ligi

“Wachezaji wanaoruhusiwa kucheza Ngao ya Jamii ni wale ambao usajili wao umekamilika tu, ambao wameshasajiliwa kucheza Ligi Kuu Tanzania Bara na michuano ya kimataifa na hakutokuwa na dakika za nyongeza kwa mechi zote, kuanzia za Nusu Fainali, Fainali hadi kusaka Mshindi wa tatu, zikiisha dakika 90, zitapigiana mikwaju ya penalti,” alisema Ofisa Habari huyo

Agosti 13, 2022, Fiston Mayele alifunga mabao yote mawili, Yanga ikiichapa Simba 2-1 katika mechi ya Ngao ya Jamii, lakini baadaye iligundulika alikuwa hajakamilisha usajili kitu kilichosababisha kutocheza mechi za awali za Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huo.

Aliitaja kanuni nyingine ni kwamba, mchezaji yeyote ambaye alimaliza Ligi Kuu msimu uliopita akiwa na kadi nyekundu au adhabu ya kusimamishwa hata mechi moja kwa kuwa na kadi tatu za njano na hakuzitumikia kwa sababu Ligi ilikuwa imemalizika, hatoruhusiwa kucheza kwani atatakiwa kutumikia adhabu yake

TPLB Yaondoa Dakika za Nyongeza Ngao ya Jamii 2024

“Kanuni hizi zinatumika pia kwenye Ligi Kuu. Kwa hiyo hata adhabu zinaingiliana, mchezaji mwenye kadi na hakutumikia hatatusubiri mpaka ligi hivyo atazitumikia kwenye Ngao ya Jamii. Lakini yeyote ambaye atapata kadi nyekundu kwenye michezo hiyo, ataitumikia pia kwenye michezo ya ligi,” alisema

Alisema wameamua kuanika baadhi ya kanuni hizo kutokana na mashabiki wengi kuwa na mkanganyiko hasa inapokuwa michezo kama hiyo ambayo ni ya mtoano, wasijue nini kinafuata baada ya timu kutoka suluhu.

Aidha michezo ya Ngao ya Jamii itaanza kupigwa Agosti 8, 2024, mchezo wa kwanza ukipigwa kati yabAzam FC dhidi ya Coastal Union Kuanzia Saa 10:00 jioni kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar.

Mchezo mwingine siku hiyo hiyo utakuwa kati ya Simba SC dhidi ya Yanga kuanzia saa 1:00 Usiku Kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Jijini Dar es Salaam.

Mchezo wa Fainali ya Ngao ya Jamii utawakutanisha washindi wa michezo ya Nusu Fainali na Fainali itapigwa Agosti 11,2024 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar Es Salaam.

PATA NYIMBO ZOTE MPYA BONYEZA HAPA

MATANGAZO YA BIASHARA WASILIANA NASI KUPITIA nijuzehabariblog@gmail.com

SHARE THIS POST:

Tags:

Comments are closed.