KUITWA KWENYE USAILI NEC 2024 TAZAMA HAPA


RATIBA KAMILI NA MAKUNDI YA EURO 2024 TAZAMA HAPA


WALIOCHAGULIWA KIDATO CHA TANO 2024 TAZAMA HAPA


FOMU ZA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2024 TAZAMA HAPA


PATA AJIRA MBALIMBALI KILA SIKU BONYEZA HAPA

UFAHAMU Ugonjwa wa PID

Filed in Makala, Afya Yako, Michezo by on 04/05/2024 0 Comments

UFAHAMU Ugonjwa wa PID

UFAHAMU Ugonjwa wa PID, Maambukizi ya via vya uzazi vya mwanamke ni nini?Dalili za ugonjwa wa uchochezi wa pelvic, Mziwaziwa na PID, Sindano ya kutibu pid, Dalili za pid,Dalili na madhara ya pid,Kirefu cha pid,Pid kwa mama mjamzito, Je karafuu inatibu pid,Metronidazole inatibu PID,Tofauti ya pid na uti,Aloe vera inatibu PID,PID treatment Kit.

UFAHAMU Ugonjwa wa PID

UFAHAMU Ugonjwa wa PID, Maambukizi ya via vya uzazi vya mwanamke ni nini?Dalili za ugonjwa wa uchochezi wa pelvic, Mziwaziwa na PID, Sindano ya kutibu pid, Dalili za pid.

Maambukizi ya via vya uzazi vya mwanamke au ugonjwa wa PID (pelvic inflammatory disease) ni maambukizi ya bakteria kwenye shingo ya uzazi, mirija ya fallopio, ovari na tumbo la uzazi (uterasi).

Sababu kuu ya ugonjwa huu kutokea ni maambukizi yanayosambazwa kwa kujamiiana (STI). Ugonjwa huu unaweza kuwaathiri wanawake wenye umri wowote, lakini wale wenye umri kati ya maika 15 na 24 huathirika zaidi.

Dalili huweza kujumuisha: maumivu ya nyonga au tumbo, maumivu wakati wa kujamiiana, na uchafu usio wa kawaida kutoka ukeni pamoja na homa.

PID hutibiwa kwa antibiotiki, na utambuzi na matibabu ya mapema ni muhimu katika kuzuia madhara ya kupata makovu na utasa.

Vihatarishi vya ugonjwa wa PID
Maambukizi ya via vya uzazi vya mwanamke ni semi ya kitabibu inayoelezea maambukizi ya shingo ya uzazi, tumbo la uzazi na mirija ya fallopio.

Kwa kawaida maambukizi haya husababishwa na bakteria.

Ingawa mara nyingi ni maamkubizi yanayosambazwa kwa njia ya kujamiiana (STI), kama vile klamidia au kisonono, wakati mwingine maambukizi haya huweza kusababishwa na bakteria wengine.

PID inaweza kuwaathiri wanawake wenye umri wowote, lakini wale wenye umri kati ya miaka 15 and 24 huathirika zaidi.

Dalili za PID
Dalili huweza kujumuisha:

  • Maumivu kwenye nyonga na tumbo
  • Maumivu wakati wa kujamiiana
  • Kutokwa damu nyingi wakati wa hedhi
  • Kutokwa na majimaji yasiyo ya kawaida ukeni
  • Baadhi ya watu huweza kupata homa, kichefuchefu, kutapika au maumivu wakati wa kujisaidia.

Utambuzi
Utambuzi mara nyingi huweza kufanywa kulingana na dalili na uchunguzi wa sehemu za siri.

Wakati wa uchunguzi, sampuli za majimaji au usaha huchukuliwa ili kutambua bakteria anayesababisha maambukizi.

Matibabu (PID treatment)
Maambukizi ya via vya uzazi vya mwanamke hutibiwa kwa antibiotiki.

Na tiba ya PID hutofautiana kulingana na ukali wa maambukizi. Ikiwa maambukiz ni makali, inaweza kuhitajika kupewa antibiotiki kupitia mishipa ya damu.

Ikiwa maambukizi husababisha usaha kukusanyika au makovu kwenye mirija ya fallopio, basi upasuaji huweza kuhitajika ingawa hii ni nadra sana.

Ubashiri
Watu wengi hupona vizuri baada ya matibabu na maambukizi hayasababishi matatizo ya muda mrefu.

Hata hivyo, ikiwa maambukizi hayatatibiwa, au ikiwa mtu anayapata maambukizi haya tena baada ya kutibiwa, basi kuna uwezekano mkubwa wa kupata madhara zaidi.

Haya huweza kujumuisha makovu kwenye tumbo la uzazi na mirija ya fallopio, ugumu wa kupata mimba, mimba kutungwa nje ya tumbo la uzazi, na maumivu ya muda mrefu ya nyonga.

Kinga
Njia muhimu ya kuzuia maambukizi ya via vya uzazi vya mwanamke ni kutumia kondomu wakati wa kujamiiana.

Kondomu ni njia bora ya kuzuia kupata maambukizi yanayosambazwa kwa njia ya kujamiiana (STIs).

Watu waliotambuliwa kuwa na STI wanapaswa kuwataarifu wapenzi wao ili wapimwe na kutibiwa pia.

KUPATA NAMBA YA NIDA BURE BONYEZA HAPA


KUOMBA LESENI YA BIASHARA BONYEZA HAPA


KUPATA TIN NUMBER BURE BONYEZA HAPA


KUOMBA LOSS REPORT BURE BONYEZA HAPA

MATANGAZO YA BIASHARA WASILIANA NASI KUPITIA [email protected]

Tags: , , , , , , , , , , , ,

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *