RATIBA YA LIGI KUU YA NBC 2024/2025 TAZAMA HAPA


INEC RATIBA YA UBORESHAJI WAPIGA KURA 2024/2025 HAPA


INEC KUITWA KWENYE USAILI 2024/2025 TAZAMA HAPA


AJIRA MPYA KILA SIKU TAFADHALI BONYEZA HAPA


JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP HAPA


USAJILI Augustine Okejepha Atua Simba

Filed in Usajili, Michezo by on 06/07/2024
SHARE THIS POST:

JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA

USAJILI Augustine Okejepha Atua Simba

USAJILI Augustine Okejepha Atua Simba

USAJILI Augustine Okejepha Atua Simba

USAJILI Augustine Okejepha Atua Simba,Augustine Okajepha ni Mnyama, rasmi Klabu ya Simba imekamilisha usajili wa kiungo mkabaji, Augustine Okajepha raia wa Nigeria kutoka Rivers United kwa mkataba wa miaka mitatu.

Okajepha ni mchezaji kijana mwenye umri wa miaka 20 aliyetunukiwa kipaji kikubwa katika idara ya kiungo wa ulinzi.

Katika miaka kadhaa Simba imekuwa ikihitaji kupata mchezaji ambaye ataipa uimara safu yetu ya ulinzi na Okajepha anatarajiwa kuwa suluhisho.

Okajepha ndiye mchezaji bora wa msimu uliopita wa Ligi Kuu nchini Nigeria (MVP) msimu wa 2023/2024.

2023/24 Okajepha amefunga bao moja
akisaidia kupatikana mabao matatu huku mara mbili akiibuka mchezaji bora wa mwezi pamoja na kujumuishwa kwenye kikosi bora cha msimu.

Moja ya sifa kubwa ya Okajepha ni kuhakikisha eneo la ulinzi linakuwa salama muda wote wa mchezo pamoja na kupiga safi na kwenda mbele na kuongeza mashambulizi.

USAJILI Augustine Okejepha Atua SimbaUbora na umri wake ni miongoni mwa sifa zilizo wavutia Simba kuhitaji saini yake wakiamini atakuwa msaada mkubwa kwa timu kuelekea msimu ujao wa Ligi wa 2024/2025.

Msimu uliopita Okajepha amechaguliwa mara mbili katika kikosi bora cha wiki cha Kombe la Shirikisho barani Afrika.

Augustine Okejepha, anakuwa mchezaji wa saba kusajiliwa na Simba kuelekea msimu ujao wa Ligi wa 2024/2025 baada ya kukamilisha usajili wa Wachezaji wengine ambao ni;

Valentino Mashaka Kutoka Geita Gold FC, Abdulrazack Mohamed Hamza kutoka Super Sport ya Afrika Kusini, Lameck Lawi kutoka Coastal Union, Joshua Mutale kutoka Power Dynamos, Steven Mukwala kutoka Asante Kotoko na Jean Charles Ahoua kutoka Stella Club d’Adjamé.

PATA NYIMBO ZOTE MPYA BONYEZA HAPA

MATANGAZO YA BIASHARA WASILIANA NASI KUPITIA nijuzehabariblog@gmail.com

SHARE THIS POST:

Tags:

Comments are closed.