USAJILI Debora Fernandes Mavambo Atua Simba
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA
USAJILI Debora Fernandes Mavambo Atua Simba
USAJILI Debora Fernandes Mavambo Atua Simba, Kiungo Debora Fernandes Mavambo mwenye uraia pacha wa Congo Brazaville lakini anachezea timu ya taifa ya Gabon amejiunga Simba kwa mkataba wa miaka mitatu akitokea Mutondo Stars ya Zambia.
Debora mwenye umri wa miaka 24 anamudu pia kucheza kama kiungo mkabaji namba sita ingawa anafurahi zaidi kucheza juu kidogo yaani namba nane.
Ujio wa Debora unaongeza nguvu katika eneo la kiungo Cha Simba kwakuwa anaweza kuzuia na kupiga pasi sahihi kuelekea mbele na kuanzisha mashambulizi.
Debora anakuwa mchezaji wa pili kusajiliwa katika idara ya kiungo wa kati baada ya kumsajili Augustine Okajepha lengo likiwa ni kuongeza uimara wa kikosi.
Pia anakuwa Mchezaji wa Nane kusajiliwa na Simba kuelekea msimu ujao wa Ligi wa 2024/2025 baada ya kukamilisha usajili wa Wachezaji wengine ambao ni;
Augustine Okejepha Kutoka Rivers United, Valentino Mashaka Kutoka Geita Gold FC, Abdulrazack Mohamed Hamza kutoka Super Sport ya Afrika Kusini, Lameck Lawi kutoka Coastal Union, Joshua Mutale kutoka Power Dynamos, Steven Mukwala kutoka Asante Kotoko na Jean Charles Ahoua kutoka Stella Club d’Adjamé.