USAJILI Duke Abuya ni Mwananchi
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA
USAJILI Duke Abuya ni Mwananchi
USAJILI Duke Abuya ni Mwananchi, Kiungo mshambuliaji Duke Abuya amejiunga na Young Africans SC kama Mchezaji huru kutoka Singida Black Stars zamani Ihefu SC.
Nyota huyo mzaliwa wa Eldoret nchini Kenya, mbali ya kuwa na uwezo wa kucheza kiungo wa kati, pia anaweza kutokea pembeni katika kupeleka mashambulizi.
Msimu uliopita Abuya alicheza mechi 28 kati ya 30 akitumia dakika 2339 ndani ya Ligi Kuu ya NBC na akahusika kwenye jumla ya magoli 8 kutokana na kufunga manne na asisti nne.
Abuya mwenye umri wa miaka 30 anakuwa mchezaji mpya wa sita kutambulishwa ndani ya Young Africans kuelekea msimu ujao wa 2024/2025 baada ya Clatous Chama SC, Prince Dube, Chadrack Boka, Khumeiny Aboubakar na Aziz Andambwile.
Uongozi wa klabu ya Yanga unaoongozwa na Rais Eng. Hersi Said bado unaendelea kuimarisha kikosi hicho kulingana na ripoti ya benchi la ufundi chini ya Kocha Mkuu, Miguel Gamondi.
Mbali na kusajili Wachezaji mapya, pia baadhi ya nyota waliokuwepo msimu uliopita ambao mikataba yao ilimalizika wamebakishwa kwa kuongezewa mikataba.
Wachezaji hao ni Aboutwalib Mshery, Djigui Diarra, Kibwana Shomari, Nickson Kibabage, Bakari Mwamnyeto, Farid Mussa na Stephane Aziz Ki.