USAJILI Omary Omary Atua Simba
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA
USAJILI Omary Omary Atua Simba
USAJILI Omary Omary Atua Simba,Klabu ya Simba SC imekamilisha usajili wa kiungo mshambuliaji, Omary Omary kutoka Mashujaa FC kwa mkataba wa miaka miwili.
Omary ni mchezaji kijana mwenye umri wa miaka 19 ambaye ana uwezo wa kucheza nafasi tofauti Uwanjani, akiwa na uwezo wa kucheza kwa ufasaha namba 8, 10, 11 na 7.
pia Omary ni kijana mwenye kipaji kikubwa jambo ambalo Simba inaamini atakuwa msaada wa timu kuelekea msimu mpya wa mashindano 2024/2025.
USAJILI Omary Omary Atua SimbaAidha mipango ya klabu hiyo ni kusajili wachezaji wenye uwezo mkubwa huku ikizingatia umri kwa kuwa inajenga timu imara ya muda mrefu.
Omary anakuwa Mchezaji wa tisa kusajiliwa na Simba kuelekea msimu ujao wa Ligi wa 2024/2025 baada ya kukamilisha usajili wa Wachezaji wengine ambao ni;
Debora Fernandes Mavambo Kutoka Mutondo Stars ya Zambia, Augustine Okejepha Kutoka Rivers United ya Nigeria, Valentino Mashaka Kutoka Geita Gold FC na Abdulrazack Mohamed Hamza kutoka Super Sport ya Afrika Kusini.
Wengine ni Lameck Lawi kutoka Coastal Union, Joshua Mutale kutoka Power Dynamos, Steven Mukwala kutoka Asante Kotoko na Jean Charles Ahoua kutoka Stella Club d’Adjamé.