USAJILI Yusuph Kagoma ni Mnyama
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA
USAJILI Yusuph Kagoma ni Mnyama
USAJILI Yusuph Kagoma ni Mnyama, Klabu ya Simba imekamilisha usajili wa Kiungo mkabaji, Yusuph Kagoma kwa mkataba wa miaka mitatu kutoka Singida Fountain Gate.
Kagoma ni moja ya vijana wazawa wenye uwezo mkubwa wa kuzuia timu ikishambuliwa na kupandisha mashambulizi.
Uwezo wake na umri wake ni miongoni mwa vigezo vya Simba kutafuta saini yake ikiwa matarajio makubwa kutoka kwake.
Kagoma yupo kwenye mipango ya maboresho makubwa ya kuirejesha timu katika ubora ambao mashabiki wengi wa Simba wanatamani kuiona.
Malengo ya Uongozi wa Simba ni kuhakikisha wanakuwa na kikosi imara kitakachokuwa na uwezo wa kuturejeshea mataji makubwa ambayo wameyapoteza katika miaka ya karibuni.
Yusuph Kagoma anakuwa Mchezaji wa 12 kusajiliwa na Simba kuelekea msimu ujao wa Ligi wa 2024/2025 baada ya kukamilisha usajili wa Wachezaji wengine ambao ni;
Karaboue Chamou Kutoka Racing Club d’ Abidjan ya Ivory Coast, Valentin Nouma kutoka St. Eloi Lupopo ya DR Congo, Omary Omary Kutoka Mashujaa FC, Debora Fernandes Mavambo Kutoka Mutondo Stars ya Zambia, Augustine Okejepha Kutoka Rivers United ya Nigeria, Valentino Mashaka Kutoka Geita Gold FC na Abdulrazack Mohamed Hamza kutoka Super Sport ya Afrika Kusini.
Wengine ni Lameck Lawi kutoka Coastal Union, Joshua Mutale kutoka Power Dynamos, Steven Mukwala kutoka Asante Kotoko na Jean Charles Ahoua kutoka Stella Club d’Adjamé.