UWAYEZU Francois Regis CEO Mpya Simba
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA
UWAYEZU Francois Regis CEO Mpya Simba
UWAYEZU Francois Regis CEO Mpya Simba, Uwayezu Francois Regis raia wa Rwanda anatajwa kuwa mrithi wa Imani Kajula katika nafasi ya Afisa Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Simba SC.
Mkataba wa Imani Kajula unatarajiwa kumalizika mwezi ujao na Simba haijaonyesha nia ya kuendelea kubaki naye.
Awali kulikuwa na jitihada za kumrejesha Barbara Gonzalez ambaye alisema kuwa hayuko tayari kurejea kutokana na sababu za Kifamilia.
Taarifa zaidi zinasema kuwa mazungumzo kati ya Simba na Francois yamefika hatua nzuri kilichobaki ni kufikia muafaka wa kumalizana naye ili aweze kuiongoza Simba kuanzia Msimu wa 2024/2025.
Francois, kwa sasa ni Makamu Mwenyekiti wa APR ya Rwanda pia amewahi pia kuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Soka cha Rwanda (FERWAFA)