VAR Kuanza Kutumika Ligi Kuu Bara 2024/2025
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA
VAR Kuanza Kutumika Ligi Kuu Bara 2024/2025
VAR Kuanza Kutumika Ligi Kuu Bara 2024/2025,Var nbc premier league today,NBC Premier League match today,
Var nbc premier league fixtures,Var nbc premier league results,Var nbc premier league live.
Waziri wa Fedha, Dk Mwigulu Nchemba amesema kuwa kuanzia msimu ujao wa Ligi Kuu Bara, Viwanja vitakavyotumika kwa Michuano hiyo Vitafungwa Teknolojia inayomsaidia Mwamuzi kufanya marejeo ya picha (Video Assistance Referee-VAR) kwaajili ya kuhakikisha matokeo yanayopatikana yanakuwa ya haki.
Amesema kuwa katika kuhakikisha hilo linafanikiwa, Serikali inakusudia kuwasilisha pendekezo la kuondoa kodi kwenye vifaa vinavyotumika kwenye teknolojia hiyo kuanzia mwaka mpya wa fedha 2024/2025.
Dk Mwigulu ameyasema hayo leo Alhamisi, Juni 13, 2024 wakati akisoma bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka mpya wa fedha 2024/2025.
“Tunataka matokeo yawe ya haki, sio kuna timu msimu unaisha imepewa penalti zaidi ya 10 na wengine mabao yao yanakataliwa, hivyo msimu ujao tunakwenda kutumia VAR,” amesema Dk Mwigulu
VAR ni nini?
Vitu gani vinaangaliwa na Video Referee Assistance?
- Magoli – ikiwa kulikuwa na ukiukwaji wa sheria wakati wa awamu ya kushambulia, kama vile faulo na Offside.
- Maamuzi ya penati – pengine si sahihi.
- Maamuzi ya moja kwa moja ya kadi nyekundu (kadi ya pili ya njano haipatikani)
- Kadi nyekundu na Kutambua makosa (mistake identity)
Namna gani VAR inafanya kazi?
VOR ni Video Operation Room ni chumba maalumu ambacho AVAR anakaa ambapo anakuwa na mtu anaitwa RO huyu ni Replay Operator, hawa wakina AVAR ni refa tu kama wengine so hawezi au ana ufinyu kujua kuhusu na mitambo ya kurusha mpira kwahiyo RO anamsaidia kufanya marejeo ya tukio analohitaji kuliona, pia OFR maana yake ni On-field referee mwamuzi wa kati ambaye anachezesha mechi.
Angalia hiyo picha hapo juu ni mwaka 2014 ambapo Oxlade Chamberlain alishika mpira kwa mkono lakini kwa bahati mbaya refa alimpatia kadi nyekundu Kieran Gibbs, maana ake hiyo ni error ya OFR lakini kule AVAR atafanya review ambapo akijua kama maamuzi sio sahihi kadi inafutwa anapatiwa anayestahili.
Namna gani wanawasiliana?
Hapo tumeongelea hilo tukio sasa ni vipi wanawasiliana ni kwamba kama refa wa kati (OFR) atakuwa hana uhakika atamuuliza AVAR kuhusu hilo tukio, na AVAR akiwa kimya maana ake OFR yuko sahihi na maamuzi aliyotoa hii ni “silent check” na kama akigundua kuna makosa atamuambia ili kumsahisha.
Kama tukio limetokea na VAR imemuambia refa wa kati kuwa kuna tatizo hili refa wa kati anakuwa na machaguo matatu kwanza ni anaweza kubadili maamuzi yake na kufuata VAR, pili kama akiona inamtatiza uwanjani kuna sehemu panaitwa Referee Review Area (RRA) hapo ataenda kuangalia marudio ya tukio akiwa na Review assistant (RA) au chaguo lake la tatu ni kusema nina amini maamuzi yangu so haendi kuangalia video.
Vitu gani VAR inasaidia goli likifungwa?
Nimesema kuwa VAR inaangalia vitu vinne kwanza goli, pili penati, tatu kadi nyekundu na makosa (mistake identity).
Kwa upambe wa goli VAR inaangalia vitu kama kabla ya goli kufungwa kulikuwa na offside kama iliwepo goli linakataliwa, kabla ya goli kufungwa mpira ulitoka? ikiwa ndio goli linakatiliwa, je kuna faulo ilifanyika kabla ya kufunga? na wakati huu haya maamuzi yanaweza kuchukua kama sekunde 30-40.
Matumizi ya VAR katika kadi nyekundu hapa inafanya kati kwa zile direct red card maana yake kama ni kadi ya njano VAR haihusiki hata ikiwa ni kadi ya pili ya njano, na kuna instance ambapo VAR ina mshauri refa hapa kwanza uigaji, kufunga goli kwa mkono, na ikigundulika umemrudishia mwenzako (kisasi).
Kwa upande wa penati inaonyesha kama mchezaji kafanyiwa faulo nje au ndani ya eneo la kumi na nane. Kama refa ataenda kuangalia review ya video akaona kuna penati basi atanyoosha vidole viwili, baada ya kidole kikubwa kinachofuatia na ataonyesha alama ya mstatili (rectangle) afu atatoa penati, hii ina maana kuwa ameona kwenye VAR.
Nini kitatokea endapo wachezaji au kocha atamzonga refa?
Kama mchezaji atasema aende kwenye video ambayo refa anaenda kuangalia, refa ana haki ya kumpa kadi ya njano na hii ata kama ni mchezaji wa akiba atapata kadi ya njano, na kama kocha atasema akamsonge refa kwenye VAR ya uwanjani basi ataonywa na kama atatoka kwenye kiboksi chake kwa mita tatu atatolewa uwanjani so ataenda back stage.
Kwa mara ya kwanza kutumia kwa VAR katika mechi ya uingereza ni Brighton vs Crystal Palace FA Cup ndio walianza kutumia hii teknolojia.
Lakini kwa dunia nzima ilitumika katika mchezo wa Major League Soccer lakini pia ilitumika mwaka 2016 katika fainali za Club world cup,lakini nchini Australia ndio ligi ya kwanza kutumia mfumo huu katika professional league.
PATA NYIMBO ZOTE MPYA BONYEZA HAPA
MATANGAZO YA BIASHARA WASILIANA NASI KUPITIA nijuzehabariblog@gmail.com
Tags: NBC Premier League match today., VAR Kuanza Kutumika Ligi Kuu Bara 2024/2025, Var nbc premier league fixtures, Var nbc premier league live., Var nbc premier league results, Var nbc premier league today