RATIBA YA LIGI KUU YA NBC 2024/2025 TAZAMA HAPA


INEC RATIBA YA UBORESHAJI WAPIGA KURA 2024/2025 HAPA


INEC KUITWA KWENYE USAILI 2024/2025 TAZAMA HAPA


AJIRA MPYA KILA SIKU TAFADHALI BONYEZA HAPA


JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP HAPA


VAR Kutumika Ligi Kuu Bara Msimu 2024/2025

Filed in Michezo by on 23/03/2024
SHARE THIS POST:

JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA

VAR Kutumika Ligi Kuu Bara Msimu 2024/2025

VAR Kutumika Ligi Kuu Bara Msimu 2024/2025,VAR kutumika Ligi Kuu Bara 2024/25,VAR Kuanza Kutumika Ligi Kuu ya NBC 2024/2025, VAR Kutumika Kwa Mkapa 2024/2025.

VAR Kutumika Ligi Kuu Bara Msimu 2024/2025

VAR Kutumika Ligi Kuu Bara Msimu 2024/2025,VAR kutumika Ligi Kuu Bara 2024/25,VAR Kuanza Kutumika Ligi Kuu ya NBC 2024/2025, VAR Kutumika Kwa Mkapa 2024/2025.

TEKNOLOJIA ya Kuwasaidia Waamuzi wa soka wawapo uwanjani (VAR) inatarajiwa kuanza kutumika katika mechi za Ligi Kuu Tanzania bara kuanzia msimu ujao wa 2024/2024 imefahamika.

RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia, aleleza hayo hivi karibuni akisema vifaa vya kiteknolojia kwaajili ya kuwasaidia waamuzi vilivyopo nchini na vyengine vitakavyoingizwa vitaimarisha eneo la utoaji maamuzi na kuondoa malalamiko.

Aidha rais huyo amewakaribisha wadau wa soka na Ligi hiyo kutoa maoni ya kanuni ya kuzikata timu pointi ambazo wachezaji au mashabiki wake wataonekana kufanya vitendo vinavyoashiria ushirikina na kuingia uwanjani wakati mechi inaendelea.

Pia amewatama wadau kutoa maoni kuhusiana na mchakato wa kuiruhusu Al Hilal ya Sudan kushiriki Ligi Kuu Tanzania Bara kuanzia msimu ujao wa 2024/2024.

Karia aliongeza kuwa wameshapokea nyaraka kutoka Shirikisho la Soka Afrika (CAF), kwaajili ya vifaa vya VAR ambapo kabla ya hapo kutakuwa na mafunzo kwa waamuzi ya namna ya kuvitumia ili mpango huo uwe na ufanisi.

“Ndiyo, tayari CAF wametusaidia wanatuletea VAR katika ule mpango wake wa kusaidia ‘zone’ zake, lakini kwanza kutakuwa na mafunzo ya jinsi ya kuitumia, tumeshapokea nyaraka, na tuko katika  mchakato wa kuomba kusamehewa kodi serikalini kabla kupokea ule mzigo wenyewe wa vifaa kabla ya kufungwa,” amesema Karia.

Mbali na VAR itakayoletwa kwa msaada wa CAF, Karia amesema wadhamini wao waliochukua jukumu la kuonyesha mpira kwenye televisheni nao wamemwahidi kununua mashine inayotembea, hivyo Tanzania kutakuwa na VAR mbili, ingawa alisema inabidi kanuni za Ligi zirekebishwe kwani baadhi ya mechi zitakuwa zinachezwa bila kifaa hicho.

Rais huyo amesema VAR inayotembea itaanza kufanyiwa majaribio katika mashindano ya Kombe la Chalenji kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), yatakayofanyika kuanzia mwezi June 29 hadi July 14, mwaka huu huko Zanzibar.

“Wadhamini wetu wanaoonyesha mpira kwenye televisheni nao wamesema watanunua VAR inayotembea, yenyewe itakuwa inahamishika, inaweza kuwa uwanja huu leo, kesho ikaenda kutumika kwenye uwanja mwingine, ile ya CAF yenyewe itafungwa kwenye Uwanja wa Mkapa, kwa hiyo itatumika hapo tu na hii ya kuhamishika itakwenda Tanga au Morogoro,” Karia amesema.

Ameongeza kuwa ni lazima zitengenezwe kanuni kwa sababu haiwezekani katika mechi nane, ni michezo mwili tu ndizo iwe na VAR na mechi nyingine zichezwe kavu.

Ameeleza kuwa kanuni zitakazotungwa ndizo zitatoa mwongozo kwa VAR hizo mbili zitumike vipi, lakini kwa anavyoona kwa kiasi kikubwa zinaweza kutumika katika michezo inayohusu Simba na Yanga pale zinapokuwa kwenye viwanja viwili tofauti.

“Mara nyingi mechi zinazotusumbua ni zile ambazo wanacheza hawa wakubwa (Simba na Yanga), wanashindana  wenyewe, kila mmoja anaweka watu wake kwaajili ya kurekodi makosa ya waamuzi yanayomnufaisha mwenzake na kurusha, huwezi kuona mechi ya Coastal na Ihefu makosa ya waamuzi yanarushwa na kujadiliwa katika mitandao ya kijamii,” ameongeza Karia.

Amesema imefika wakati wa kuwalinda waamuzi wa Kitanzania ambao wanaheshima katika mashindano ya kimataifa yanayosimamiwa na CAF kwa kuwaletea VAR.

“Wenzetu wanawalinda sana marefa wao, wanafanya mambo ya ajabu sana, waamuzi ni binadamu, wengine wanapitiwa, wengine wanafanya makusudi, lakini wanalindwa, pia wanasaidia wa VAR, kwetu likifanyika tu tunawarushia Dunia nzima,” amesema kiongozi huyo.

VAR Kutumika Ligi Kuu Bara Msimu 2024/2025

VAR ni nini?

VAR (Video Referee Assistance) hii ni teknolojia ambayo imeletwa na chama cha marefa kupitia International Football Association Board (IFAB), ikiwa na lengo la kusahisha refa wa kati katika maamuzi yake kupitia video.
Kwa sasa mechi nyingi zinakuwa na waamuzi wanne namaanisha refa wa kati, ma-lines men wawili pamoja na fourth official, japokuwa kuna baadhi ya michuano kunakuwa na marefa nyuma ya magoli.
Kutokana na makosa ya kibinadamu chama cha maamuzi wasaidizi waliomba hii kuwepo kwa refa wa tano ambaye yeye atakaa katika Video akiwa na haedsett kwaajili ya kuwasiliana na refa wa kati.

Vitu gani vinaangaliwa na Video Referee Assistance?

Kwa sasa teknolojia hii ya VAR inaonyesha mapitio ya Vitu vinne, ambavyo ni
  1. Magoli – ikiwa kulikuwa na ukiukwaji wa sheria wakati wa awamu ya kushambulia, kama vile faulo na Offside.
  2. Maamuzi ya penati – pengine si sahihi.
  3. Maamuzi ya moja kwa moja ya kadi nyekundu (kadi ya pili ya njano haipatikani)
  4. Kadi nyekundu na Kutambua makosa (mistake identity)

Namna gani VAR inafanya kazi?

Kwa kutofautisha kuna vifupisho nitatumia ili ulichanganye, VAR ni Video referee assistance maaana yake ni ile kamera inayorekodi tukio, wakati AVAR kirefu chake ni Assistant Video Assistance Referee ikiwa na maana kuwa ni yule mtu ambaye anaopareti na VAR na kumuambia refa wa kati.

VOR ni Video Operation Room ni chumba maalumu ambacho AVAR anakaa ambapo anakuwa na mtu anaitwa RO huyu ni Replay Operator, hawa wakina AVAR ni refa tu kama wengine so hawezi au ana ufinyu kujua kuhusu na mitambo ya kurusha mpira kwahiyo RO anamsaidia kufanya marejeo ya tukio analohitaji kuliona, pia OFR maana yake ni On-field referee mwamuzi wa kati ambaye anachezesha mechi.

Mchezaji wa Arsenal OXlade Chamberlain aligusa mpira kwa mkonokatika mchezo dhidi ya chelsea

Mchezaji wa Arsenal OXlade Chamberlain aligusa mpira kwa mkono
katika mchezo dhidi ya chelsea

Angalia hiyo picha hapo juu ni mwaka 2014 ambapo Oxlade Chamberlain alishika mpira kwa mkono lakini kwa bahati mbaya refa alimpatia kadi nyekundu Kieran Gibbs, maana ake hiyo ni error ya OFR lakini kule AVAR atafanya review ambapo akijua kama maamuzi sio sahihi kadi inafutwa anapatiwa anayestahili.

Namna gani wanawasiliana?

Hapo tumeongelea hilo tukio sasa ni vipi wanawasiliana ni kwamba kama refa wa kati (OFR) atakuwa hana uhakika atamuuliza AVAR kuhusu hilo tukio, na AVAR akiwa kimya maana ake OFR yuko sahihi na maamuzi aliyotoa hii ni “silent check” na kama akigundua kuna makosa atamuambia ili kumsahisha.

AVAR akimuambia OFR nini kinatokea

AVAR akimuambia OFR nini kinatokea?

Kama tukio limetokea na VAR imemuambia refa wa kati kuwa kuna tatizo hili refa wa kati anakuwa na machaguo matatu kwanza ni anaweza kubadili maamuzi yake na kufuata VAR, pili kama akiona inamtatiza uwanjani kuna sehemu panaitwa Referee Review Area (RRA) hapo ataenda kuangalia marudio ya tukio akiwa na Review assistant (RA) au chaguo lake la tatu ni kusema nina amini maamuzi yangu so haendi kuangalia video.

Vitu gani VAR inasaidia goli likifungwa?

Nimesema kuwa VAR inaangalia vitu vinne kwanza goli, pili penati, tatu kadi nyekundu na makosa (mistake identity).

Kwa upambe wa goli VAR inaangalia vitu kama kabla ya goli kufungwa kulikuwa na offside kama iliwepo goli linakataliwa, kabla ya goli kufungwa mpira ulitoka? ikiwa ndio goli linakatiliwa, je kuna faulo ilifanyika kabla ya kufunga? na wakati huu haya maamuzi yanaweza kuchukua kama sekunde 30-40.

Matumizi ya VAR katika kadi nyekundu hapa inafanya kati kwa zile direct red card maana yake kama ni kadi ya njano VAR haihusiki hata ikiwa ni kadi ya pili ya njano, na kuna instance ambapo VAR ina mshauri refa hapa kwanza uigaji, kufunga goli kwa mkono, na ikigundulika umemrudishia mwenzako (kisasi).

Hii ni penati baada ya kuangalia kwenye video assistance referee hii ndio ishara inayotumika kuchora mstatili hewani

Hii ni penati baada ya kuangalia kwenye video assistance referee hii ndio ishara inayotumika kuchora mstatili hewani

Kwa upande wa penati inaonyesha kama mchezaji kafanyiwa faulo nje au ndani ya eneo la kumi na nane. Kama refa ataenda kuangalia review ya video akaona kuna penati basi atanyoosha vidole viwili, baada ya kidole kikubwa kinachofuatia na ataonyesha alama ya mstatili (rectangle) afu atatoa penati, hii ina maana kuwa ameona kwenye VAR.

Nini kitatokea endapo wachezaji au kocha atamzonga refa?

Kama mchezaji atasema aende kwenye video ambayo refa anaenda kuangalia, refa ana haki ya kumpa kadi ya njano na hii ata kama ni mchezaji wa akiba atapata kadi ya njano, na kama kocha atasema akamsonge refa kwenye VAR ya uwanjani basi ataonywa na kama atatoka kwenye kiboksi chake kwa mita tatu atatolewa uwanjani so ataenda back stage.

Kwa mara ya kwanza kutumia kwa VAR katika mechi ya uingereza ni Brighton vs Crystal Palace FA Cup ndio walianza kutumia hii teknolojia.

Lakini kwa dunia nzima ilitumika katika mchezo wa Major League Soccer lakini pia ilitumika mwaka 2016 katika fainali za Club world cup,lakini nchini Australia ndio ligi ya kwanza kutumia mfumo huu katika professional league.

PIA UNAWEZA KUSOMA👇

PATA NYIMBO ZOTE MPYA BONYEZA HAPA

MATANGAZO YA BIASHARA WASILIANA NASI KUPITIA nijuzehabariblog@gmail.com

SHARE THIS POST:

Tags: , , ,

Comments are closed.