VIINGILIO Yanga vs Vital’O FC August 24-2024
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA
Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Yanga SC, Ali Kamwe amewataka mashabiki na Wanachama wa timu hiyo kujitokeza kwa wingi kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa Jumamosi katika mchezo wa pili wa hatua ya awali Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Vital’O FC ya Burundi.
Ali Kamwe amesema kuwa Yanga imepania kupeleka ujumbe Barani Afrika kwa kujaza uwanja wa Benjamin Mkapa katika mechi za hatua ya awali.
Aidha Kamwe amewaahidi Wananchi kuwa siku hiyo watakwenda kujaza kapu la mabao ili kuhakikisha wanaondoka na fedha za kutosha kutokana na goli la Mama.
Kamwe ametangaza viingilio vya mchezo huo kuwa Mzunguuko na Machungwa itakuwa Tsh 5,000/-, kwa VIP C itakuwa Tsh 10,000/-, VIP B itakuwa Tsh 20,000/-, na VIP A ni Tsh 30,000/-
“Tiketi tayari zimeanza kuuzwa, nawaomba Wananchi tununue tiketi mapema tuache mazoea ya kununua tiketi siku za mwisho ili kuepuka changamoto zisizotarajiwa,” alisema Kamwe