VYAMA vya Siasa Kuweka Wakala Vituo vya Kuandikisha Wapiga Kura July 01-2024
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA
VYAMA vya Siasa Kuweka Wakala Vituo vya Kuandikisha Wapiga Kura July 01-2024
VYAMA vya Siasa Kuweka Wakala Vituo vya Kuandikisha Wapiga Kura July 01-2024, Vyama vya siasa vitaruhusiwa kuweka wakala mmoja kwenye kila kituo cha kuandikisha wapiga kura kwenye uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura unaotarajiwa kuzinduliwa mkoani Kigoma tarehe 01 Julai 2024.
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Mhe. Jaji (Rufaa), Jacobs Mwambegele wakati akifungua mkutano wa Tume na viongozi wa vyama vya siasa uliofanyika jijini Dar es Salaam tarehe 07 Juni, 2024 ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya uboreshaji wa Daftari.
“Leo kila chama kitapewa nakala ya orodha ya vituo vyote vya kuandikisha wapiga kura. Dhumuni la kuwapatia nakala hizo ni kuwawezesha kupanga na kuweka mawakala wa uandikishaji katika vituo vya kuandikisha wapiga kura,” amesema na kuongeza….
“Kila chama kitaruhusiwa kuweka wakala mmoja kwenye kituo cha kuandikisha wapiga kura kwa lengo la kushuhudia utekelezaji wa zoezi la uboreshaji kituoni ikiwemo kuwatambua wale wanaokuja kituoni kama wana sifa za kuandikishwa”.
Jaji Mwambegele amesema kwamba kikao hicho ni sehemu ya utamaduni wa Tume iliojiwekea wa kuwashirikisha wadau wa uchaguzi wakati wa utekelezaji wa majukumu yake.
Aliwataja wadau hao kuwa ni pamoja na Viongozi wa vyama vya siasa, Viongozi wa Dini, Wawakilishi wa Asasi za Kiraia, Wahariri wa Vyombo vya habari, Waandishi wa habari, Maafisa Habari wa Mikoa na Halmashauri, Wawakilishi wa Makundi mbalimbali ya Vijana, Watu wenye ulemavu na wanawake.
” Niwaombe Viongozi wa Vyama vya Siasa kwa umoja wenu kuzingatia sheria za uchaguzi, kanuni za uboreshaji na maelekezo ya Tume kuhusu zoezi la uboreshaji wa Daftari. Tume kwa upande wetu tutazingatia Katiba, sheria ya uchaguzi na kanuni zilizotungwa chini ya sheria katika zoezi hili la uboreshaji,” amesema.
Kwenye mkutano huo, Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Bw. Kailima, R. K amesema kuwa pamoja na kufanyika kwa uzinduzi tarehe 01 Julai, 2024 mkoani Kigoma ambapo Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (MB), uboreshaji wa Daftrai utaanza siku hiyo mkoani kigoma na kuendelea kwa siku saba hadi tarehe 07 Julai, 2024.
”Kwa lengo la kutekeleza jukumu hilo kwa ufanisi, uboreshaji utafanyika kwenye mizunguko 13 itakayobainishwa kwenye ratiba. Aidha, zoezi hili litaendeshwa kwa siku saba kwenye kila kituo cha kuandikisha wapiga kura,” amesema.
PATA NYIMBO ZOTE MPYA BONYEZA HAPA
MATANGAZO YA BIASHARA WASILIANA NASI KUPITIA nijuzehabariblog@gmail.com
Tags: VYAMA vya Siasa Kuweka Wakala Vituo vya Kuandikisha Wapiga Kura July 01-2024