WACHEZAJI wa Yanga hawa mbioni Kuachwa
WACHEZAJI wa Yanga hawa mbioni Kuachwa
WACHEZAJI wa Yanga hawa mbioni Kuachwa, Klabu ya Young Africans tayari imeanza Mazungumzo ya kuwaongezea mikataba mipya baadhi ya Wachezaji ambao mikataba Yao inatamatika na wanahitajika klabuni.
Aidha Wachezaji wengine ambao hawahitaji hawataongezwa mikataba na badala yake wataachwa Ili watafute timu zingine!
Twende tukaone Wachezaji ambao watabaki na watakaoachwa Kuelekea msimu ujao wa 2024/2024.
Farid Mussa, huyu mkataba wake unatamatika mwishoni mwa msimu huu ila mpaka muda huu hakuna mazungimumzo yoyote yaliyoanza.
Zawadi Mauya, pia mkataba wake unatamatika mwishoni mwa msimu huu ila imefahamika kuwa Klabu ya Yanga haina Mpango wa kuendelea kuwa naye.
Denis Nkane, Mwisho wa Msimu huu atakuwa Mchezaji huru na imefahamika kuwa klab yake ya Yanga haina Mpango naye tena.
Nickson Kibabage, Tayari ameshaongeza mkataba mpya wa miaka 3 baada ya ule wa Mkopo kutamatika.
Clement Mzize, Mkataba wake ulikuwa unaelekea ukingoni ila tayari ameshaongeza kandarasi ya miaka 2.
Makudubela Skudu, huyu Mwamba tayari ametaarifiwa kuwa klabu hiyo hakina mpango naye kuelekea Msimu ujao wa 2024/2025.
Kibwana Shomari, Mkataba wake na Yanga unaelekea ukingoni ila Mazungumzo ya mkataba mpya yameanza licha ya kuwa tayari ana ofa 3 mkononi mwake.
Bakari Mwamnyeto, Mazungumzo ya mkataba mpya yameanza na muelekeo wake ni mzuri, pia alikuwa na ofa za vilabu viwili mkononi mwake.
Joyce Lomalisa, Mkataba wake unaelekea tamati na hakuna mazungumzo yoyote ya kuongeza mkataba mpya mpaka muda huu.
Metacha Mnata, Mkataba yake na unaelekea mwishoni kabisa ila bado hakuna mazungumzo ya mkataba mpya.
Pacome Zouzoua, Mwamba huyu amesaliwa na mkataba wa mwaka mmoja ila Young Africans imepanga kumuongezea miaka mingine miwili.
Aziz Ki, Mkataba wake ukiwa ukingoni taarifa za ndani ya uongozi wa Yanga zinadai alishaongeza mkataba Mpya.
Aidha Kuna Uwezekano wa Wachezaji Wazawa wasiopungua watatu kuachwa baada ya mikataba yao kuisha pia wapo wa kigeni wasiopungua 4 ili kupisha maingizo mapya.
Imefahamika kuwa Klabu hiyo imepanga kusajili wachezaji wasiopungua wanne (4) wa kigeni, washambuliaji wawli, kiungo mmoja na Mlinzi wa kushoto Mmoja.