WACHEZAJI Walioachwa Simba 2024/2025
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA
WACHEZAJI Walioachwa Simba 2024/2025
WACHEZAJI Walioachwa Simba 2024/2025, Wachezaji Walioachwa na Simba 2024/2025,Wachezaji Walioachwa Simba SC 2024/2025, Wachezaji Walioachwa na Klabu ya Simba 2024/2025, Wachezaji waliopewa Thank You Simba SC 2024/2025.
Wakati dirisha Kubwa la Usajili Ligi Kuu ya NBC msimu wa 2024/2025 lililofunguliwa Juni 15 likitarajiwa kufungwa Agosti, 31 saa 5:59 usiku, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limesisitiza kuwa hakutakuwa na muda wa ziada baada ya dirisha hilo kufungwa.
Kutokana na taarifa hiyo kutoka TFF timu zinapaswa kukamilisha usajili ndani ya muda ikiwa ni pamoja na uhamisho wa Kimataifa (ITC) kwa wachezaji wanaotoka nje ya nchi.
Kuelekea dirisha hilo kufungwa Nijuze Habari inakuletea Wachezaji ambao wameachwa na Klabu ya Simba Sports Club Kuelekea Msimu Mpya wa 2024/2025.
Klabu ya Simba Sc imetangaza kuachana na mchezaji wake na nahodha Mkuuz John Bocco baada ya kutoridhishwa na mwendelezo wa ubora wake ingali John ameshakuwa kocha wa timu ya vijana ya Simba.
Nyota huyo ameitumikia Simba kwa kipindi cha miaka 7 na anakuwa wa Mchezaji kwanza kupewa THANK YOU katika fagio la Chuma linalotarajiwa kupita Msimbazi kwenye dirisha hili kubwa la Usajili la 2024/2025.
Uongozi wa klabu Simba SC umetangaza kuachana na mchezaji, Saido Ntibazonkiza raia wa Burundi baada ya mkataba wake kumalizika.
Katika kipindi cha mwaka mmoja na nusu alichodumu Simba akitokea Geita Gold FC, Ntibazonkiza amekuwa mchezaji muhimu wa kikosi cha kwanza akiwa mfungaji bora wa timu katika misimu yote miwili na klabu inathamini mchango wake.
Mshambuliaji, Shaban Idd Chilunda amemaliza mkataba wake wa mwaka mmoja Simba SC, hivyo hatokuwa sehemu ya kikosi cha Simba kuelekea msimu mpya wa mashindano wa 2024/2025, Simba imeeleza.
Klabu ya Simba imefikia Maamuzi ya kutomuongezea Mkataba Kiungo mshambuliaji, Luis Jose Miquissone baada ya mkataba wake kumalizika.
Kwa jinsi hiyo Miquissone anaungana na John Bocco, Saido Ntibanzonkiza, Shaban Idd Chilunda kupewa Thanks You na Klabu hiyo.
Baada ya miaka mitano aliyodumu ndani ya klabu Simba SC, mlinzi wa kati Kennedy Wilson Juma hatokuwa sehemu ya kikosi Klabu hiyo kuelekea msimu mpya wa 2024/2025 baada ya mkataba wake kumalizika.
Kwa jinsi hiyo Kennedy Juma anaungana na John Bocco, Saido Ntibanzonkiza, Shaban Idd Chilunda na Luis Jose Miquissone kupewa Thanks You na Klabu hiyo.
Baada ya kuitumikia timu Simba kwa misimu mitatu, Henock Inonga Baka hatokuwa sehemu ya kikosi hicho cha msimu ujao wa 2024/2025 baada ya kuuzwa kwenda FA Rabat inayoshiriki Ligi Kuu nchini Morocco.
Klabu ya Simba imetangaza kuachana Kiungo Mkabaji, Sadio Kanoute baada ya makubaliano ya pande zote mbili.
Kanoute alijiunga na Simba msimu wa 2021/22 akitokea klabu ya Al Ahly Benghazi ya nchini Libya.
Klabu ya Simba umefikia makubaliano ya kuvunja mkataba na Mshambuliaji, Pa Omar Jobe baada ya kipindi kifupi cha miezi sita.
Jobe raia wa Gambia mwenye umri wa miaka 25 alijiunga na Simba katika dirisha la usajili la mwezi Januari akiwa mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba wake na timu ya Zhenis inayoshiriki Ligi Kuu nchini Kazakhstan.
Wachezaji Aishi Manula, Israel Mwenda na Leandre Esomba Onana wameachwa rasmi na Simba SC.
Simba Sports Club ni timu ya soka iliyo na makao makuu katika mtaa wa Msimbazi, Kariakoo, katika jiji la Dar es Salaam nchini Tanzania inayoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara ambapo ilianzishwa mwaka 1936, ikiitwa kwanza Eagles na baadaye tena iliitwa Dar Sunderland.
Mwaka 1971 ikaibadilisha jina lake kabisa na kuitwa, Simba Sport Club (ambalo linamaanisha Lion kwa Kiinɡereza).
Simba Sports Club ni mojawapo ya timu kubwa ya mpira wa miguu nchini Tanzania, wapinzani wao karibu ni Younɡ Africans.
Ni mabingwa wa taifa mara 18 tena ni mabingwa mara 6 katika kombe la Kagame, kwenye Ligi Kuu ni Mabingwa mara 22.
Mechi zao za nyumbani Simba wanatumia viwanja viwili, ambavyo ni Uwanja wa Uhuru na Uwanja wa Taifa.
PATA NYIMBO ZOTE MPYA BONYEZA HAPA
MATANGAZO YA BIASHARA WASILIANA NASI KUPITIA nijuzehabariblog@gmail.com
Tags: Wachezaji Walioachwa na Klabu ya Simba 2024/2025, Wachezaji Walioachwa na Simba 2024/2025, WACHEZAJI Walioachwa Simba 2024/2025, Wachezaji Walioachwa Simba SC 2024/2025, Wachezaji waliopewa Thanks Simba SC 2024/2025.