WACHEZAJI Waliopewa Thank You Azam FC 2024/2025
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA
WACHEZAJI Waliopewa Thank You Azam FC 2024/2025
WACHEZAJI Waliopewa Thank You Azam FC 2024/2025, Klabu ya Azam FC imetangaza kuachana na Wachezaji wake Wanne ambao ni Ayoub Lyanga, Edward Manyama, Malickou Ndoye na Issa Ndala ambao mikataba yao imefikia ukomo.
Taarifa ya Azam Fc imesema: “Ahsanteni sana kwa mchango wenu wa kuipigania nembo ya klabu yetu kwa kipindi chote mlichokuwa nasi. Tunawatakia kila la kheri huko muendako katika safari yenu nyingine ya soka.”
Aidha Azam FC tayari imempa Thank You aliyekuwa beki na nahodha wake, Daniel Amoah mwenye umri wa miaka 26, ambaye amedumu klabuni hapo tangu 2016 akitokea Medeama SC ya kwao Ghana.