WAFANYABIASHARA 891 Waliokidhi Vigezo vya Kurejeshwa Soko la Kariakoo
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA
WAFANYABIASHARA 891 Waliokidhi Vigezo vya Kurejeshwa Soko la Kariakoo
WAFANYABIASHARA 891 Waliokidhi Vigezo vya Kurejeshwa Soko la Kariakoo, Orodha Ya Wafanyabiashara 891 Waliokidhi Vigezo Vya Kurejeshwa Kufanya Biashara Katika Soko la Kariakoo Baada ya Mradi Kukamilika.
Shirika la Masoko ya Kariakoo linautangazia umma orodha kamili ya
majina ya wafanyabiashara wenye sifa na vigezo vya kurejeshwa sokoni
Kariakoo baada ya ujenzi wa soko jipya na ukarabati wa soko kuu
kukamilika.
Taarifa hii pia inapatikana katika tovuti ya Ofisi ya Rais –TAMISEMI www.tamisemi.go.tz na Shirika la Masoko ya Kariakoo www.kariakoomarket.co.tz.
Orodha hii pia imebandikwa kwenye mbao za matangazo zilizopo kwenye Soko la Machinga Complex na Soko la Kisutu.
Wafanyabiashara wanaodaiwa na Shirika ambao wapo kwenye orodha
hii wanajulishwa kuwa hawatarejeshwa sokoni hadi watakapolipa madeni
ya kodi waliyolimbikiza kwa muda mrefu.
Shirika hilo limetoa kipindi cha mwezi
mmoja kuanzia leo tarehe 10 Julai 2024 hadi tarehe 09 Agosti 2024 kwa
wadaiwa wote kukamilisha malipo ya madeni yao.
Kwa wafanyabiashara wenye hoja au maoni kuhusu majina yao kutoonekana kwenye Orodha ya uhakiki, Shirika linatoa muda wa siku tatu
kuanzia tarehe 11 hadi 13 Julai 2024 kuwasilisha madai yao.
Maafisa wa Shirika watakuwepo katika viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam kuanzia saa 3.00 asubuhi hadi saa 9.00 alasiri kusikiliza na kutoa ufafanuzi kwa wafanyabiashara.
DOWNLOAD PDF HAPA KUPATA ORODHA KAMILI
PATA NYIMBO ZOTE MPYA BONYEZA HAPA
MATANGAZO YA BIASHARA WASILIANA NASI KUPITIA nijuzehabariblog@gmail.com
Tags: WAFANYABIASHARA 891 Waliokidhi Vigezo vya Kurejeshwa Soko la Kariakoo