WALIOGUSWANA na Bomba la Mafuta Ghafi Kagera Wapigwa Msasa Kuboresha Maisha yao, Uchumi na Maendeleo
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA
WALIOGUSWANA na Bomba la Mafuta Ghafi Kagera Wapigwa Msasa Kuboresha Maisha yao, Uchumi na Maendeleo
WALIOGUSWANA na Bomba la Mafuta Ghafi Kagera Wapigwa Msasa Kuboresha Maisha yao, Uchumi na Maendeleo, Walioguswa na Mradi wa ujenzi wa Bomba la mafuta ghafi Mkoani Kagera unaohusisha nchi za Afrika Mashariki wa (ECOP) East Africa Oil Pipeline utakaokuwa unasafirisha mafuta Ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi chongeleani mkoa wa Tanga nchini Tanzania ambapo bomba hilo litazikwa chini ya Ardhi lenye urefu wa kilometa 1443 walioguswa Mkoani humo tayari wameendelea kujengewa uwezo wa namna ya kujikimu kimaisha katika Kilimo,ufugaji pamoja na Biashara.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi huo wilayani Muleba Mkoani Kagera Haji Kihwele ambaye ni kiongozi wa timu ya mipango wa ulejeshaji wa hali ya kimaisha ya walioguswa katika mikoa ya Kagera na Geita kupitia Mradi wa mafuta ghafi (ECOP) E360 Julai 10 mwaka 2024 amesema kuwa afla hii ya saba imekutanisha viongozi mbalimbali wa kiserikali kuanzia ngazi za Vijiji, vitongoji halmashauri,Mkoa,watekelezaji pamoja na waguswa wa bomba la Mafuta ghafi ambapo mradi huo umetenga hali ya ulejeshaji wa Mali kwa familia zilizoguswa katika zoezi la utoaji wa Ardhi ili kupisha mradi wa bomba la mafuta ghafi Afrika Mashariki na kuepuka utoaji wa Ardhi usilete athari hasi kwa waguswa wa mradi ambapo mradi umeanza ulejeshaji wa usawa kimaisha kwa waguswa.
Kwa upande wake Charles Shagi ambaye ni Mratibu wa Uhusiano wa Jamii wa mradi wa mafuta ghafi (ECOP) amesema kuwa kuanzishwa kwa Mradi huo nchi ya Uganda bomba litakuwa na urefu wa kilometa 296 na Tanzania Bomba litakuwa na urefu wa kilometa 1147 ambapo mikoa nane itanufaika,wilaya 24 Halmashauri 27 ambapo Mkoa wa Kagera utapita kwenye Halmashauri nne.
Shagi amesema kuwa walioguswa na mradi huo kwa Kagera ni watu 2196 katika wilaya nne za Missenyi, Bukoba, Muleba, na Biharamulo katika wilaya inayoongoza ni Muleba inajumla ya watu 1209 katika maeneo waliyokuwemo wanatarajia kujenga miundombinu saidizi katika wilaya za Missenyi na Muleba na kujenga kituo cha musukuma mafuta.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera hajjat Fatma Mwassa ameushukuru uongozi wa mradi huo wa mafuta ghafi kwa kutenga muda wa kutoa elimu ya Biashara kwa walioguswa na mradi kwa kurejesha hali ya Mali kwa waguswa katika Wilaya ya Muleba ambapo amesema mbinu hizi za Biashara zitakuwa msingi wa kuboresha rasilimali tunazozalisha na kuwa faida zikiwemo ufugaji wa nyuki,Kilimo na matarajio yake kutoka kwa waguswa kufanikiwa kwa kupata tija,kuinuka kiuchumi na kimaendeleo kutokana na elimu waliyoipa.
Mwassa ametoa wito kwa viongozi wa dini kuwa mstari wa mbele kutoa elimu kwa waumini wao kuchangamkia fursa za kibiashara.
PATA NYIMBO ZOTE MPYA BONYEZA HAPA
MATANGAZO YA BIASHARA WASILIANA NASI KUPITIA nijuzehabariblog@gmail.com
Tags: Uchumi na Maendeleo, WALIOGUSWANA na Bomba la Mafuta Ghafi Kagera Wapigwa Msasa Kuboresha Maisha yao