WANAFUNZI Kaya Maskini Kupata Mkopo Elimu ya Juu Asilimia 100
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA
WANAFUNZI Kaya Maskini Kupata Mkopo Elimu ya Juu Asilimia 100
WANAFUNZI Kaya Maskini Kupata Mkopo Elimu ya Juu Asilimia 100, MFUKO wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) umeweka Mazingira ya kuwezesha Wanafunzi wote wanaojiunga na Elimu ya Juu kutoka kaya maskini, kupata mkopo kwa asilimia 100 ili watimize ndoto zao.
Katika kipindi cha miaka mitatu kuanzia 2021/22, wanafunzi 4,600 wamenufaika kutokana na TASAF kuwatambulisha kwa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB).
Hayo yalielezwa jana na Mkurugenzi wa Mifumo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) wa TASAF, Justine Boaz, alipozungumza na waandishi wa habari waliotembelea wanufaika wa mfuko huo katika wilaya za Arusha na Moshi.
Alisema wanafunzi kutoka kaya zinazoishi katika umaskini uliokithiri, wanapata mkopo kwa asilimia 100 kwa kozi yoyote chuo kikuu.
“Na kwa sasa tumeongea na HESLB ili watoto wanaotoka kaya maskini wapate mikopo mara tu chuo kinapofunguliwa badala ya kusubiri wiki mbili au tatu. Nia ni kuwezesha kufika chuo kwa wakati na kuwaepushia usumbufu.
“Tupo katika hatua za mwisho kuhakikisha hili linafanikiwa na tayari mifumo yetu inasomana na bodi. Mwanzoni tulikuwa tunawapa barua ya utambulisho lakini sasa hivi tunataka wakishathibitishwa tu chuoni, bodi inawasoma na kuwapatia mkopo,” alisema mkurugenzi huyo.
Mmoja wa wanufaika wa TASAF, Caroline Minja wa Mtaa wa Kariwa Chini, Kata ya Rau, Manispaa ya Moshi, alisema mtoto wake ni miongoni mwa wanufaika wa mfumo huo na sasa anasoma Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori Mweka.
Takwimu za serikali zinaonesha asilimia nane ya Watanzania wanaishi katika lindi la umaskini, wakishindwa kumudu milo mitatu kwa siku.
Dhima kuu ya Dira ya Maendeleo ya Taifa ni kupunguza walau nusu ya wananchi wanaoishi katika umaskini na kuwafanya waishi katika uchumi wa kati ifikapo 2025, yaani mwakani.
PATA NYIMBO ZOTE MPYA BONYEZA HAPA
MATANGAZO YA BIASHARA WASILIANA NASI KUPITIA nijuzehabariblog@gmail.com
Tags: WANAFUNZI Kaya Maskini Kupata Mkopo Elimu ya Juu Asilimia 100