KUITWA KWENYE USAILI NEC 2024 TAZAMA HAPA


RATIBA KAMILI NA MAKUNDI YA EURO 2024 TAZAMA HAPA


WALIOCHAGULIWA KIDATO CHA TANO 2024 TAZAMA HAPA


FOMU ZA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2024 TAZAMA HAPA


PATA AJIRA MBALIMBALI KILA SIKU BONYEZA HAPA

WAOMBA Ajira za Polisi Walalamikia Mtandao

Filed in Ajira, Michezo by on 20/05/2024 2 Comments

WAOMBA Ajira za Polisi Walalamikia Mtandao

WAOMBA Ajira za Polisi Walalamikia Mtandao

WAOMBA Ajira za Polisi Walalamikia Mtandao

WAOMBA Ajira za Polisi Walalamikia Mtandao, Baada ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni kuongeza siku tano za kuomba ajira Polisi zinazoisha Kesho Jumanne ya May 21-2024, Malalamiko ya Ugumu wa kufunguka Kwa mtandao wa Kuomba Ajira hizo yameendelea kutolewa kupitia maoni ya wasomaji kwenye akaunti ya X zamani Twitter ya Jeshi la Polisi.

Malalamiko hayo yametolewa na watu mbalimbali huku wengine wakishauri jeshi hilo liruhusu barua za maombi zipelekwe kwa mkono kwa Makamanda wa Polisi wa Mikoa na Wilaya.

Malalamiko ya watu hao yako kwenye maoni ya taarifa za polisi kwenye akaunti yao ya ‘Police Force TZ’ iliyopo kwenye mtandao wa X.

May 15-2024, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni alitangaza kuongeza siku tano za kuomba ajira kwenye Jeshi la Polisi ambazo siku yake ya mwisho awali ilikuwa May 16-2024.

Masauni alisema hayo baada ya kutolewa hoja na Mbunge wa Makete, Festo Sanga aliyetumia kanuni namba 54 ya kutoa jambo la dharura bungeni, kwamba kukosekana kwa mtandao wa intaneti nchini (wakati huo) kungewakosesha fursa vijana kwa kushindwa kutuma maombi ya kazi.

Licha ya kuongezwa siku tano, Masauni pia alisema iwapo changamoto ya intaneti itaendelea, Serikali itaangalia namna ya kufanya ili kuwasaisia waombaji kufikia lengo.

Hizi siku mlizoongeza ili watu wafanye maombi ni bora mngeziongeza baada ya kufanya marekebisho ya mtandao wenu kwanza. Siku zinaisha changamoto inaendelea kuwepo what is this ?

Malalamiko yaliyopo kwenye maoni ya taarifa za polisi anasema; ‘Hivi ‘link’ ya ajira itaanza kufunguka lini? Na siku ndo zinakaribia kuisha’

Mlalamikaji mwingine anasema, Mfumo bado changamoto. Na hamtoi taarifa yoyote shida nini?

Mwingine anasema, link ya kutuma maombi haifunguki sisi tulio na internet cafe wateja hawatuelewi, wanadhani tunawatapeli, toeni hata neno kwamba mfumo wenu umeshindwa kukabiriana na changamoto iliyojitokeza, mtusaidie, wateja wanatuona wezi wa kimtandao kwa hiki kinachoendelea.’

Mlalamikaji mwingine ni yeye anasema ‘Hizi siku mlizoongeza ili watu wafanye maombi ni bora mngeziongeza baada ya kufanya marekebisho ya mtandao wenu kwanza. Siku zinaisha changamoto inaendelea kuwepo what is this (Hii nini nini)?

Mlalamikaji mwingine anasema, ‘Wakuu mfumo haujakaa sawa kabisa unagoma kabisa kufunguka.

Mwingine, anasema ‘Mfumo wa maombi ya ajira unagoma kufunguka, fanyeni namna ya kurekebisha hili.’

Kwenye Channel yetu ya WHATSAPP ndani ya saa 1 watoa maoni asilimia kubwa wameonesha mtandao wa kutuma maombi haufunguki bado na asilimia nyingine wanaonesha wameshindwa kabisa kutuma hata pale mtandao ulipofunguka, asilimia ndogo kabisa ndio waliofanikiwa kutuma maombi hayo.

KUPATA NAMBA YA NIDA BURE BONYEZA HAPA


KUOMBA LESENI YA BIASHARA BONYEZA HAPA


KUPATA TIN NUMBER BURE BONYEZA HAPA


KUOMBA LOSS REPORT BURE BONYEZA HAPA

MATANGAZO YA BIASHARA WASILIANA NASI KUPITIA [email protected]

Tags:

Comments (2)

Trackback URL | Comments RSS Feed

  1. Jamani nikiwanaomba kamakunauwezekano kamanda mkuu wapolisi ange lusu waombaji tupeleke maombi kwa mkuu wajeshi mkowa kupitiya barua zilizo andikwa kwasisi vijana maana tunaangaika mtandaosana Bado haujafunguka naskundozimeisha Jaman tinaomba watoweneno kwahilo swala

  2. Juma khatibu Juma says:

    Jamani mtandao unasumbua kwangu tuh au hadi kwenu unasumbua maana naona haufunguki tangu maomni yalivyo anza kutangazwa

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *