Wawili Yanga Kuikosa Kagera Sugar
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA
Klabu ya Young Africans imethibitisha kuikosa huduma beki wake kulia, Yao Kouassi kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Kagera Sugar utakaopigwa kesho Alhamisi Kuanzia Saa 11:00 jioni kwenye uwanja wa Kaitaba, Mkoani Kagera.
Mwingine ambaye Young Africans imethibitisha kuikosa huduma yake kwenye mchezo wa kesho ni Farid Mussa ambapo wachezaji hao hawakusafiri na timu kutokana na kuwa majeruhi.
Katika hali nyingine, klabu hiyo imewasili salama mkoani Kagera kuelekea mchezo huo.
Yanga imepata mapokezi makubwa kutoka kwa mashabiki wake waliojitokeza kwa wingi uwanja wa ndege wa Bukoba.