Willy Onana apishana na Moussa Camara Simba
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA
Willy Onana apishana na Moussa Camara Simba
Willy Onana apishana na Moussa Camara Simba,Ujio wa golikipa mpya kutoka Horoya Athletic Club ya kwaoGuinea, Moussa Camara umemfanya winga Willy Esomba Onana kung’oka Msimbazi baada ya taarifa kuvuja kuwa yeye ndiye anayempisha kipa huyo aliyetua kuziba nafasi ya Ayoub Lakred aliyeumia kambini nchini Misri.
Usajili wa Camara ndani ya Simba umekuwa wa dharura kutokana na kuumia kwa Ayoub Lekred, ambaye ndiye golikipa tegemeo ndani ya kikosi hicho.
Kusajiliwa Kwa Camara kunaifanya Simba kuwa makipa wanne ambao wengine ni Hussein Abel, Ally Salim pamoja naAyoub Lakred
Katika mazoezi ya mwisho ya timu hiyo, yaliyofanyika Ijumaa Agosti 2, 2024, Uwanja wa Benjamin Mkapa, Onana hakuwa sehemu ya kikosi na taarifa za ndani zinaeleza keshapata timu huko Qatar anayoweza kujiunga nayo muda wowote.