Wydad yamfuata Clement Mzize
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA
Klabu ya Wydad Athletic ya nchini Morocco imewasilisha ofa kwenye klabu ya Young Africans ili kuona kama itamsajili Mshambuliaji, Clement Mzize.
Taarifa kutoka ndani ya uongozi wa Yanga imethibitisha kuwa Wydad wamewasilisha ofa yao ya kwanza ambayo hata hivyo imekataliwa kwa sababu haijafikia thamani halisi ya mchezajim
Young Africans imegoma kupokea takribani Tsh Milioni 270 (dola 100,000) huku wakiweka msimamo wa kuhitaji takribani Bil 2.7 kumuachia Mzize ambaye aliibuliwa katika kikosi cha Yanga U20 kabla ya kupandishwa timu ya wakubwa miaka miwili iliyopita.
Clement Mzize ni miongoni mwa washambuliaji muhimu katika kikosi cha Yanga msimu huu, hivo haitakuwa rahisi kumuachia akaondoka kwa dau dogo.