YANGA kucheza na Kaizer Chiefs Kombe la Toyota
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA
YANGA kucheza na Kaizer Chiefs Kombe la Toyota
YANGA kucheza na Kaizer Chiefs Kombe la Toyota, Klabu ya Young Africans imepata mwaliko wa kucheza mchezo maalum wa Kombe la Toyota dhidi ya Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini.
Mchezo huo umepangwa kuchezwa Julai 28, 2024 huu kwenye Uwanja wa Toyota uliopo Bloemfontein nchini Afrika Kusini.
Taarifa iliyotolewa na Kaizer Chiefs ambayo sasa inafundishwa na Kocha Nasreddine Nabi, imeeleza kwamba:
“Kaizer Chiefs watakuwa wenyeji wa Young Africans katika mchuano wa kwanza wa Kombe la Toyota utakaochezwa kwenye Uwanja wa Toyota mjini Bloemfontein mnamo tarehe 28 Julai 2024.”
Aidha Rais wa Young Africans, Eng. Hersi Said, amezungumzia mwaliko huo kwa kusema: “Kama Young Africans SC, tunafurahishwa sana na mwaliko huu wa kushiriki katika Kombe la Toyota 2024.
“Mchezo huu unaendeleza uhusiano kati ya timu hizo ambao ulianza mwaka jana Yanga walipowaalika Kaizer Chiefs kushiriki katika Tamasha la Wiki ya Mwananchi. Tunafurahia mwaliko huu na tunaahidi kutoa mchezo wa ushindani utakaotusaidia kujiandaa kwa msimu mpya wa 2024/25.”