YANGA Kufanya Mkutano Mkuu wa Mwaka Leo June 09-2024
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA
YANGA Kufanya Mkutano Mkuu wa Mwaka Leo June 09-2024
YANGA Kufanya Mkutano Mkuu wa Mwaka Leo June 09-2024, Klabu ya Yanga inatarajiwa kufanya Mkutano Mkuu wa mwaka wa Wanachama Leo Jumapili tarehe 09 Juni 2024.
Mkutano huo utafanyika Katika ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano (Julius Nyerere ICC) Kuanzia Saa 4:00 asubuhi na itakuwa LIVE Azam TV.
Huu ni utaratibu wa kawaida kwa kila mwisho wa wa Msimu (Kila Mwaka) Wanachama kupata taarifa muhimu kuhusu uendeshaji wa klabu yao
Pia kupitia Mkutano huo, Wanachama watafanya tathmini ya Bajeti ya mwaka uliopita 2023/2024 na kupitisha Bajeti ya mwaka mpya wa 2024/2025
Rais wa Yanga Injinia Hersi Said amewaalika Wanachama katika Mkutano huo huku akiweka bayana kuwa kutakuwa na ‘surprise’ ya aina yake kutoka kwa viongozi kabla na baada ya mkutano huo.
Hata hivyo, Hersi alitaja baadhi ya Ajenda za Mkutano huo wa kawaida kuwa ni;
- Kufungua Mkutano
- Uhakiki wa Wajumbe watakaoudhuria Mkutano.
- Kuthibitisha Ajenda
- Kuthibitisha Kumbukumbu za Mkutano uliopita
- Yatokanayo na Mkutano Uliopita.
Nijuze Habari inafahamu kuwa Mshambuliaji wa zamani wa Simba SC, Jean Othos Baleke mwenye umri wa miaka 23 yupo chini, pengine ndiye Surprise mojawapo kwenye Mkutano huo.