YANGA Kutangaza Ubingwa kwa Mtibwa Sugar?
YANGA Kutangaza Ubingwa kwa Mtibwa Sugar?
YANGA Kutangaza Ubingwa kwa Mtibwa Sugar?, Mabingwa Watetezi Ligi Kuu ya NBC Yanga leo wana nafasi ya kutwaa taji hilo kwa Msimu wa tatu Mfululizo pale watakapochuana na Mtibwa Sugar katika mchezo utakaopigwa uwanja wa Manungu, Turiani Morogoro.
Klabu hiyo inahitaji pointi mbili tu kuwaa Ubingwa hivyo Ushindi katika mchezo huo utawahakikishia Wananchi bao Ubingwa wa 30.
Mbio za ubingwa kwa Yanga zimerahisishwa na watani zao Simba ambao jana walilazimishwa sare ya bao 1-1 na Kagera Sugar.
Sare hiyo iliifanya Simba ifikishe pointi 57 ambazo ikishinda Mechi 4 zilizobaki itafikisha jumla ya pointi 69.
Kwa upande wa Azam FC ambayo imebakiwa na mechi 3 ikishinda zote pia itafikisha jumla ya pointi 69.
Kwa jinsi hiyo Yanga wakipata ushindi leo dhidi ya Mtibwa Sugar watafikisha pointi 71 ambazo haziwezi kufikiwa na Simba Wala Azam zilizopo nafasi ya 2 na ya 3.