YANGA Mabingwa Kombe la Toyota 2024
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA
YANGA Mabingwa Kombe la Toyota 2024
YANGA Mabingwa Kombe la Toyota 2024, Klabu ya Yanga imefanikiwa kutwaa taji la kwanza la msimu huu Kombe la Toyota baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya wenyeji Kaizer Chiefs, mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Toyota mjini Bloemfontein nchini Afrika Kusini.
Mabao ya Yanga kwenye mchezo huo yalifungwa na Prince Dube dakika ya 24, Stephane Aziz Ki mawili, dakika ya 45 na 62 na Clement Mzize dakika ya 57.
Baada ya mchezo huo, Aziz Ki alitangazwa kuwa Mchezaji Bora wa Mechi na kupewa mfano wa hundi ya Randi za Afrika Kusini 5000, zaidi ya Sh. Milioni 7.3 za Tanzania huku Yanga wakikabidhiwa Kombe.
Kwa mchezo huo Yanga inakamilisha mechi zake za kirafiki katika ziara yake ya wiki mbili nchini Afrika Kusini.
Mechi zingine ni dhidi ya Augsburg ya Ujerumani ambapo walifungwa mabao 2-1 na dhidi ya ya TS Galaxy ambapo walishinda 1-0.
Baada ya michezo hiyo Yanga watarejea nchini Usiku wa kuamkia Kesho Jumanne Majira ya saa 9:00 kwajili ya tamasha la Kilele ch Wiki ya Mwananchi Agosti 4-2024.
Yanga inatarajiwa kucheza dhidi ya Red Arrows ya Zambia kwenye Kilele cha Wiki ya Mwanachi Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.