Yanga tishio Afrika inajengwa – Injinia Hersi
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA
Rais wa Yanga Injinia Hersi Said amesema kuwa bado malengo ya kuijenga Yanga tishio barani Afrika hayajakamilika, hivo maboresho zaidi yanatarajiwa kufanyika katika dirisha dogo la usajili.
Hersi amesema katika dirisha hili kuna wachezaji wawili ambao waliwaweka katika mpango wa kuwasajili lakini hawakufanikiwa.
Amesema Yanga itarudi tena kwenye dirisha dogo kuwanasa nyota hao akiamini usajili wao utakwenda kukamilisha mikakati ya kuwa na kikosi tishio Afrika.
“Bado kikosi chetu hakijakamilika kuwa tishio Afrika, tunafikiria kuongeza wachezaji wawili ambao walikuwa target yetu kwenye dirisha hili kubwa lakini biashara zao hazikukamilika”
“Dirisha dogo tutarudi kuangalia kama tutaweza kukamilisha sajili zao, wakishafika ndio mtapata majibu maana ya timu kukamilika,” alisema Injinia Hersi katika mahojiano na Wasafi FM.
Soma na hii: VILABU 30 Bora Afrika 2023/2024 CAF Club Ranking