Yanga vs Vital’O FC Kupigwa Azam Complex
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA
Mchezo wa marudio kati ya Yanga dhidi ya Vital’O ya Burundi utachezwa kwenye uwanja wa Azam Complex badala ya Benjamin Mkapa kama ilivyopangwa hapo awali.
Hayo yamebainishwa na Rais wa Yanga, Mhandisi Heris Said Agosti 21, 2024 wakati akifanya mahojiano maalumu katika kipindi cha Ndani ya Jana na Leo kinachorushwa na kituo cha radio ya Wasafi.
“Kutokana na marekebisho yanayoendelea kwenye Uwanja wa Mkapa, mechi yetu ya marudiano dhidi ya Vital’O, hatutacheza tena uwanja wa Mkapa, tutacheza katika uwanja wa Azam Complex, Jumamosi majira ya saa 1:00 Usiku.
“Mechi iliyopita wenzetu Vital O walisema watatunywa kama supu lakini tulifanikiwa kupata ushindi wa goli 4, lakini kwenye mchezo huu wa marudiano ni zamu yetu sasa kuwanywa wao kama supu.”alisema Heris Said
Soma na hii: Yanga tishio Afrika inajengwa – Injinia Hersi