YANGA Waiandikia CAF Barua kukataliwa goli la Aziz Ki
YANGA Waiandikia CAF Barua kukataliwa goli la Aziz Ki
YANGA Waiandikia CAF Barua kukataliwa goli la Aziz Ki, Mkurugenzi wa Sheria na Wanachama klabu ya Yanga Simon Patrick amesema kuwa licha ya kufahamu hakuna kitakachobadilisha Matokeo ya Mchezo dhidi ya Mamelodi Sundowns lakini watumia haki yao kwa kupeleka malalamiko Shirikisho la soka Barani Afrika (CAF)
Hayo ni baada ya bao la Yanga kukataliwa katika mchezo wa mkondo wa pili Robo Fainali Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Mamelodi Sundowns.
Aidha Serikali inaunga mkono uamuzi huo wa Yanga baada ya Naibu Waziri wa Sanaa, Utamaduni na Michezo Mh Hamis Mwinjuma kubainisha kuwa baada ya mazungumzo kati yake na viongozi wa Yanga, wameona ni vyema kulalamika ili kuweka kumbukumbu sawa
Kwenye barua hiyo ambayo Yanga imeiandika kupitia kwa Mkurugenzi wake wa sheria Simon Patrick, imewalalamikia Marefa kwa kushindwa kutumia teknolojia ya VAR kupata ufumbuzi, hivyo wanaamini na kulalamika kupitia sheria namba XVI kwamba kuna viashiria vya upangaji wa matokeo ikiwemo pia kitendo cha Refa wa kati kushindwa kwenda kwenye VAR kuangalia utata wa goli hilo licha ya kwamba aliweza kwenda kwenye VAR kuhakiki faulu ya Mchezaji wa Yanga.
Pamoja na mambo mengine Yanga wameiomba CAF ichunguze tukio hilo kwa undani kwa kutumia ushahidi wa rekodi za VAR na footage za mechi ili kubaini endapo kuna viashiria vya upendeleo kwa Mamelodi vimefanyika na ikijiridhisha kuna upendeleo ichukue hatua kwa kila aliyehusika, iweke hatua madhubuti za kudhibiti tukio kama hilolisijirudie kwenye mechi zijazo na pia ichukue maamuzi mengine ambayo CAF itaona yanafaa chini sheria za mpira za CAF namba XVI kifungu namba 3.