RATIBA YA LIGI KUU YA NBC 2024/2025 TAZAMA HAPA


INEC RATIBA YA UBORESHAJI WAPIGA KURA 2024/2025 HAPA


INEC KUITWA KWENYE USAILI 2024/2025 TAZAMA HAPA


AJIRA MPYA KILA SIKU TAFADHALI BONYEZA HAPA


JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP HAPA


YANGA Yaalikwa nchi tatu Maandalizi ya Msimu 2024/2025

Filed in Michezo by on 10/06/2024
SHARE THIS POST:

JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA

YANGA Yaalikwa nchi tatu Maandalizi ya Msimu 2024/2025

YANGA Yaalikwa nchi tatu Maandalizi ya Msimu 2024/2025

YANGA Yaalikwa nchi tatu Maandalizi ya Msimu 2024/2025

YANGA Yaalikwa nchi tatu Maandalizi ya Msimu 2024/2025,Rais wa Yanga, Injinia Hersi Said, amesema kuwa timu hiyo itafanya usajili bora zaidi msimu ujao tofauti na ilivyokuwa kwa msimu uliopita wa 2023/2024.

Akizungumza katika Mkutano Mkuu wa Klabu hiyo, Hersi, amesema kwamba moja ya malengo makubwa kwao kama uongozi ni kuona wanafanya vizuri zaidi ili kukidhi mahitaji ya mashabiki na wanachama wa Klabu hiyo.

“Niwahakikishie ndugu zangu, msimu ujao tutafanya usajili mzuri ukiambatana na benchi bora la ufundi, lengo ni kufikia mafanikio ya ndani na nje ya nchi,” alisema.

Hersi aliongeza kuwa, tayari wameshapata mialiko ya zaidi ya nchi tatu kwaajili ya kuweka kambi ya maandalizi ya msimu mpya ‘Pre Seasons’.

“Tuna timu zinazotoka Ulaya ambazo zimetuomba kwenda kwao na hiyo itakuwa ni surprise (mshangao), nchi nyingine ni Kenya na Afrika Kusini ambazo tumepokea mialiko yao na tutakaa na kuifanyia kazi,”amesema.

Aidha Hersi alisema kuwa, sababu kubwa ya kupata mialiko kwa upande wa Kenya ni kwaajili ya kufungua Uwanja wao wa kisasa wa Kisumu huku kwa upande wa Afrika Kusini wakiwa wamealikwa na Kaizer Chiefs ambao msimu uliopita waliwaalika katika Kilele cha Wiki ya Mwananchi.

SOMA NA HIZI👇👇👇

PATA NYIMBO ZOTE MPYA BONYEZA HAPA

MATANGAZO YA BIASHARA WASILIANA NASI KUPITIA nijuzehabariblog@gmail.com

SHARE THIS POST:

Tags:

Comments are closed.