YANGA Yamtambulisha Mtaalam wa Tiba ya Viungo
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA
YANGA Yamtambulisha Mtaalam wa Tiba ya Viungo
YANGA Yamtambulisha Mtaalam wa Tiba ya Viungo, Klabu ya Yanga imekamilisha usajili wa Sekhwela Seroto ambaye ni Mtaalam wa Tiba ya Viungo (Physiotherapist).
Mtaalamu huyo raia wa Afrika Kusini, amekuja ndani ya Young Africans kuchukua nafasi ya Youssef Ammar, hivyo anaungana na benchi la ufundi la Young Africans linaloongozwa na Kocha Mkuu, Miguel Gamondi.
Ndani ya timu, Seroto majukumu yake makubwa ni kusaidia waliopata majeraha kupona vizuri baada ya kuumia sambamba na kuandaa na kusimamia mazoezi ya mwili
yanayotumika kama tiba.
Mbali na hayo, pia kushirikiana na wataalamu wengine kitengo cha madaktari kuhakikisha wachezaji wanakuwa salama.