YANGA Yaomboleza Kifo Cha Yusuf Manji
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA
YANGA Yaomboleza Kifo Cha Yusuf Manji
YANGA Yaomboleza Kifo Cha Yusuf Manji,Uongozi wa Klabu Young Africans Sports Club Kupitia Kurasa zake za Mitandao ya Kijamii umesema kuwa umepokea kwa mshtuko na masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha aliyewahi kuwa Mdhamini na Mwenyekiti wa Klabu hiyo, Ndug. Yusuf Manji.
Rais wa Young Africans Sports Club, Eng Hersi Said amesema kuwa enzi za uhai wake Ndugu, Yusuf Manji alikuwa kiongozi mahiri aliyejituma na kujitoa kwaajili ya kuijenga Klabu hiyo.
“Hili ni pigo kubwa kwetu Young Africans Sports Club na familia ya michezo kwa ujumla. Tutamkumbuka Yusuf Manji kwa mapenzi yake makubwa aliyokuwa nayo kwa Klabu yetu na namna alivyokuwa akijitoa kwa hali na mali katika kuiendeleza sekta ya michezo Tanzania,” amesema Rais Eng, Hersi Said.
Ndugu Yusuf Manji alihudumu katika nafasi mbalimbali za kiuongozi ndani ya Klabu kama Mdhamini na Mwenyekiti ambapo hadi umauti unamkuta alikuwa Mwanachama wa Young Africans Sports club.
Uongozi wa Young Africans Sports Club, unatoa pole kwa familia, ndugu, jamaa, marafiki na wanamichezo wote nchini kwa msiba mzito wa mpendwa wetu.
Tunamuombea kwa Mwenyezi Mungu aipumzishe roho ya Marehemu mahala pema peponi, Amina.
Sisi ni wa Mwenyezi Mungu na kwake tutarejea.
Imetolewa na
Idara ya Habari na Mawasiliano
30.06.2024