Yanga yapewa siku 45 kuilipa Benchem usajili wa Okrah
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA
Shirikisho la mpira wa miguu Duniani (FIFA) limeitaka klabu ya Young Africans kuilipa Klabu Benchem United ya nchini Ghana kiasi cha dola 80,000 (sawa na Sh 217 milioni) kutokana na usajili wa Kiungo Mshambuliaji, Augustine Okrah.
Hukumu hiyo imetolewa na FIFA jana August 19, 2024, baada ya Benchem United kufungua madai dhidi ya Young kufuatia Young Africans kusitisha mkataba wa nyota huyo.
Augustine Okrah alisajiliwa na Young Africans January 2024 katika usajili wa dirisha dogo akitokea Benchem United FC.
Kutoka na kutakuwa na wakati mzuri kikosini huku akisumbuliwa na majeraha ya mara kwa mara pamoja na masuala binafsi ya nje ya uwanja Young Africans ilifikia maamuzi ya kusitisha mkataba huku kukiwa hakuna taarifa rasmi.
Baada ya Benchem United kushinda, Young Africans imepewa siku 45 tu kukamilisha malipo hayo ili kuepuka kifungo cha kutoruhusiwa kufanya usajili.