YANGA Yazindua Wiki ya Mwanachi, Ali Kamwe Arejea
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA
YANGA Yazindua Wiki ya Mwanachi, Ali Kamwe Arejea
YANGA Yazindua Wiki ya Mwanachi, Ali Kamwe Arejea, Klabu ya Yanga leo imetangaza kuzindua wiki ya Mwananchi ambayo kilele chake kitakuwa August 04 katika uwanja wa Benjamin Mkapa, Jijini Dar Es Salaam.
Uzinduzi huo ulikwenda sambamba na urejeo wa Haji Sunday Manara ambaye anaungana na Ali Kamwe katika kitengo cha Habari na Mawasiliano.
Ali Kamwe amerejea kwenye nafasi yake ya Umeneja wa Habari na Mawasiliano baada ya kusaini Mkataba mpya wa miaka miwili ndani ya Klabu hiyo.
Uamuzi huo wa kumrejesha umefanywa na Rais wa Yanga Eng. Hersi na Makamu wake Arafat Haji baada ya Kamwe kueleza changamoto zake kwa viongozi zilizompelekea kuchukua uamuzi huo kwa maslahi ya pande zote mbili na wamekubaliana kuzifanyia kazi.
YANGA Yazindua Wiki ya Mwanachi, Ali Kamwe Arejea
Akitangaza ratiba ya wiki ya Mwananchi, Kamwe amesema kuwa kikosi cha Yanga kitawasili Alfajiri ya kesho Jumanne ambapo amewataka Wananchi kujitokeza kwa wingi kuipoikea timu na kufurahia taji walilotwaa Afrika Kusini.
Kesho Jumanne Yanga itatangaza mdhamini wa Wiki ya Mwananchi ambapo siku ya Jumatano itakuwa maalum kwaajili ya kufanya usafi katika Hospitali Mbalimbali.
Alhamisi kutakuwa na zoezi la kuchangisha damu pamoja na matukio ya hamasa ambayo yataanzia Mbagala, Zakhiem
Ijumaa Yanga itafanya dua ya Kitaifa kwaajili ya kuiombea Yanga, wachezaji, viongozi na wale wote waliotangulia mbele ya haki.
Jumamosi Makao Makuu ya Yanga kutakuwa na jogging sambamba na utaratibu wa supu utafanyika Jangwani takribani ng’ombe 20 wameandaliwa kwaajili ya zoezi hilo.