RATIBA YA LIGI KUU YA NBC 2024/2025 TAZAMA HAPA


INEC RATIBA YA UBORESHAJI WAPIGA KURA 2024/2025 HAPA


INEC KUITWA KWENYE USAILI 2024/2025 TAZAMA HAPA


AJIRA MPYA KILA SIKU TAFADHALI BONYEZA HAPA


JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP HAPA


ZAIDI ya Wapiga Kura Wapya Milioni 5 Kuandikishwa Daftari la Kudumu La Wapiga Kura

Filed in Habari by on 24/07/2024
SHARE THIS POST:

JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA

ZAIDI ya Wapiga Kura Wapya Milioni 5 Kuandikishwa Daftari la Kudumu La Wapiga Kura

Na Mariam Kagenda_Kagera

Mwakilishi wa mkurugenzi wa uchaguzi ambaye pia ni mkurugenzi wa idara ya habari na elimu ya mpiga kura Giveness Aswile

Mwakilishi wa mkurugenzi wa uchaguzi ambaye pia ni mkurugenzi wa idara ya habari na elimu ya mpiga kura Giveness Aswile

Wapiga kura wapya Milioni 5,586,433 Nchini wanatarajia kuandikishwa kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura na Tume Huru ya Taifa ya uchaguzi Nchini Tanzania (INEC) sawa na asilimia 18.7 ya Wapiga Kura 29,754,699 waliopo kwenye Daftari baada ya Uboreshaji uliofanyika mwaka 2019/2020.

Taarifa hiyo imetolewa na Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Uchaguzi kutoka Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Bi.Giveness Aswile wakati wa Mkutano wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi na Wadau wa Uchaguzi Mkoani Kagera kuhusu Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.

Bi Giveness amesema kuwa kwa mkoa wa Kagera wapiga kura wapya wanaotarajiwa kuandikishwa kwenye Daftari hilo ni 219,321 ikiwa ni ongezeko la asilimia 15.5 ya wapiga Kura 1,412,008 waliopo kwenye Daftari ambapo Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi inatarajia baada ya Uandikishaji Mkoa wa Kagera utakuwa na Wapiga Kura 1,631,329 na kwa Mkoa huo Zoezi la Uboreshaji wa Daftari utaanza tarehe 5 mpaka 11 mwezi wa 8,2024.

Wadau wa Uchaguzi Mkoani Kagera

Wadau wa Uchaguzi Mkoani Kagera

Amesema idadi hiyo inaweza kuongezeka kwa kuwa inawezekana wapo watanzania ambao walikuwa na sifa za kuandikishwa kuwa Wapiga Kura wakati wa uboreshaji wa Daftari mwaka 2019/2020 lakini kwa sababu moja au nyingine hawakuweza kujiandikisha kuwa wapiga Kura kwa sababu mbalimbali hawakuweza kujiandikisha .

Wadau wa Uchaguzi Mkoani Kagera

Wadau wa Uchaguzi Mkoani Kagera

Ameongeza kuwa zoezi hilo litahusisha kuandikisha Wapiga Kura wapya ambao ni raia wa Tanzania wenye umri wa miaka 18 na zaidi pamoja na wale watakaotimiza umri huo ifikapo tarehe ya Uchaguzi Mkuu 2025, kutoa fursa kwa Wapiga Kura waliopo kwenye Daftari na wamehama ili waweze kuhamisha taarifa zao kutoka Kata au Jimbo walipoandikishwa awali , kuondoa Wapiga Kura waliopoteza sifa za kuwemo kwenye Daftari kutokana na sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuukana uraia wa Tanzania na waliofariki.

Makamu Mwenyekiti wa Tume huru ya Taifa ya Uchaguzi Jaji wa Mahakama ya Rufani Mstaafu Mbarouk.Salim.Mbarouk akizungumza wakati wa mkutano wa tume na wadau wa uchaguzi

Makamu Mwenyekiti wa Tume huru ya Taifa ya Uchaguzi Jaji wa Mahakama ya Rufani Mstaafu Mbarouk.Salim.Mbarouk akizungumza wakati wa mkutano wa tume na wadau wa uchaguzi

Upande wa Makamu Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Mbaruku.S. Mbaruku amewataka wadau wa Tume hiyo Mkoa wa Kagera kusaidia Tume katika Uhamasishaji kwa walengwa wa zoezi hilo ili Mkoa wa Kagera utakapoanza zoezi hilo waweze kujitokeza kwa wingi kujiandikisha na kuboresha taarifa zao.

Wadau wa Uchaguzi Mkoani Kagera

Wadau wa Uchaguzi Mkoani Kagera

PATA NYIMBO ZOTE MPYA BONYEZA HAPA

MATANGAZO YA BIASHARA WASILIANA NASI KUPITIA nijuzehabariblog@gmail.com

SHARE THIS POST:

Tags:

Comments are closed.