RATIBA YA LIGI KUU YA NBC 2024/2025 TAZAMA HAPA


INEC RATIBA YA UBORESHAJI WAPIGA KURA 2024/2025 HAPA


INEC KUITWA KWENYE USAILI 2024/2025 TAZAMA HAPA


AJIRA MPYA KILA SIKU TAFADHALI BONYEZA HAPA


JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP HAPA


ZFF yatuma Maombi ya kuwa Mwenyeji CECAFA Senior Challenge 2024

Filed in Michezo by on 10/02/2024

ZFF yatuma Maombi ya kuwa Mwenyeji CECAFA Senior Challenge 2024

ZFF yatuma Maombi ya kuwa Mwenyeji CECAFA Senior Challenge 2024

ZFF yatuma Maombi ya kuwa Mwenyeji CECAFA Senior Challenge 2024

ZFF yatuma Maombi ya kuwa Mwenyeji CECAFA Senior Challenge 2024

SHIRIKISHO la Soka Zanzibar (ZFF), limethibitisha kukamilisha maombi ya kuwa mwenyeji wa mashindano ya CECAFA Senior Challenge 2024, yanayotarajiwa kufanyika mwezi July, mwaka huu 2024.

Mataifa Washindi wa tenda hizo wanatarajiwa kutangazwa katika Mkutano Mkuu wa wa Cecafa utakaoafanyika February 23, 2025 Jijini Mombasa, Kenya.

ZFF imefanya hivyo baada ya CECAFA kutangaza nafasi za kuwania kuandaa Mashindano mengine Matano yatakayofanyika mwaka 2024 ambayo ni;

  • Kuwania kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika ‘AFCON’ kwa wanaume chini ya miaka 17 na 20, (AFCON U-17 Boys qualifiers), na (AFCON U-20 Boys qualifiers).
  • Kuwania kufuzu Ligi ya Mabingwa Afrika kwa wanawake ngazi ya klabu (CAF Women’s Champions League Zonal qualifiers)
  • Kuwania Kushiriki Michuano ya kutafuta Bingwa wa Shule za Afrika (Africa Schools Football Championships Zonal qualifiers),
  • pamoja Michuano ya Ubingwa wa CECAFA kwa Wanawake chini ya umri wa miaka 20 (CECAFA U-20 Girls Championship).
ZFF yatuma Maombi ya kuwa Mwenyeji CECAFA Senior Challenge 2024

ZFF yatuma Maombi ya kuwa Mwenyeji CECAFA Senior Challenge 2024

Cecafa Senior Challenge ni miongoni mwa michuano ya muda mrefu zaidi Afrika inayoandaliwa na Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika na Kati (CECAFA), ikiwa imeanzishwa mwaka 1926 ikijulikana kama Gossage Cup na mechi ya kwanza ilipigwa mwaka huo kati ya Uganda na Kenya iliyoshinda mabao 2-1.

Mashindano hayo yanayoshirikisha nchi wanachama wa Baraza hilo na yanatambulika na Shirikisho la Soka Duniani (FIFA), ni Tanzania, Uganda, Ethiopia, Eritrea, Djibouti, Burundi, Somalia, Rwanda, Sudan na Kenya.

Mara ya mwisho kwa Michuano hiyo kufanyika ilikuwa December 2019, Uganda wakitwaa Ubingwa huo baada ya kuichapa Eritrea mabao 3-0 kwenye mechi ya Fainali iliyopigwa dimba la Lugogo, Jijini Kampala.

Wakati huo timu shiriki zilikuwa tisa, Uganda, Burundi, Djibouti, Eritrea, Kenya, Somalia, Sudan, Tanzania na Zanzibar.

PIA UNAWEZA KUSOMA👇

Tags:

Comments are closed.