SELECTION ZA FORM FIVE NA VYUO VYA KATI 2024 BONYEZA HAPA


MSIMAMO NBC PREMIER LEAGUE 2023/24 BONYEZA HAPA


RATIBA YA LIGI KUU YA NBC 2023/2024 BONYEZA HAPA


JINSI YA KUANGALIA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA FORM FIVE 2024 BONYEZA HAPA


PATA AJIRA MBALIMBALI KILA SIKU BONYEZA HAPA


IBENGE Kumrithi Benchikha Simba

Filed in New by on 07/05/2024 0 Comments

IBENGE Kumrithi Benchikha Simba

IBENGE Kumrithi Benchikha Simba

IBENGE Kumrithi Benchikha Simba

IBENGE Kumrithi Benchikha Simba, Klabu ya Simba iko katika nafasi nzuri ya Kumsajili kocha Florent Ibenge, baada ya yeye mwenyewe kuomba kuondoka Al Hilal ya Sudan, huku uongozi wa timu hiyo ukiendelea kupambana kumbakisha.

Taarifa kutoka vyanzo tofauti vya habari za michezo Afrika, zinaeleza kuwa kocha huyo amekaa vikao viwili na mabosi wa Al Hilal wakimweleza kuwa wana imani naye, lakini mwenyewe amesisitiza kuwa anataka kuondoka na sababu kubwa ni kutaka kuifundisha timu inayocheza Ligi Kuu na kupambania mataji.

“Kwenye majadiliano ya hatima yake, viongozi wamemweleza kocha kuwa bado wana imani na utendaji wa kazi yake na wanataka kuendelea naye, lakini ameng’ang’ania kuondoka kwa sababu timu kwa sasa haichezi ligi kutokana na machafuko yanayoendelea nchini Sudan,” vilisema vyanzo hivyo.

Licha ya kwamba Al Hilal huenda ikacheza Ligi Kuu Tanzania Bara nchini, baada ya maombi yao kukubaliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), lakini kocha huyo bado anaonekana hajaridhika na hilo.

Ibenge anatajwa kuwa kwenye orodha ya wanaotakiwa na Klabu ya Simba na kupewa nafasi kubwa ya kuwa kocha mkuu, baada ya kuondoka, Abdelhak Benchikha, huku kitendo cha kuomba kuondoka Al Hilal kikionekana kuwa huenda tayari ameshafikia makubaliano na klabu hiyo.

Hii si mara ya kwanza kwa klabu hiyo kumhitaji Ibenge raia wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, ilibaki kidogo imnase mwaka 2022, lakini ilishindikana na kuangukia kwa Zoran Maki.

Meneja Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Simba, Ahmed Ally, amesema kila kitu kinakwenda vizuri, lakini hivi sasa siyo wakati wa kuzungumzia kitu chochote kuhusu kocha au usajili kwani akili yao ni kusaka nafasi mbili za juu ili msimu ujao warejee kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.

“Tunaleta kocha bora, na tutafanya usajili mkubwa safari hii, mashabiki wetu watulie, kwa sasa si wakati wake, kwanza tuungane, tushikane ili kupate nafasi ya kurejea tena kule tulikozoea,” alisema Ahmed.

Alisema watafanya maamuzi magumu kwa lengo la kuiboresha timu yao na kuahidi kuwafurahisha mashabiki wao kutokana na usajili watakaoufanya.

Alisema watapitia ripoti ya benchi la ufundi lililopo chini ya Juma Mgunda pamoja na Kamati ya ufundi na kuweka wazi kuwa baada ya msimu huu kumalizika wataipitia ili wajue ni sehemu gani za kupaboresha.

“Ninaomba Wanasimba wasiwe na wasiwasi msimu ujao tutafanya mabadiliko ambayo yatamwacha wazi kila mtu, tumedhamiria makubwa tunataka turudishe heshima yetu ya mwanzo,” alisema.

KUPATA NIDA BURE BONYEZA HAPA

KUOMBA LESENI YA BIASHARA BONYEZA HAPA

KUPATA TIN NUMBER BURE BONYEZA HAPA

KUOMBA LOSS REPORT BURE BONYEZA HAPA

Tags:

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *