Simba Queens vs Kenya Police Bullets Nusu Fainali CECAFA
LICHA ya kuambulia sare ya 2-2 dhidi ya PVP Buyenzi ya Burundi tayari, Simba ambao ni wawakilishi wa Tanzania Bara katika michuano ya timu za soka za Wanawake ukanda wa CECAFA ilishafuzu Nusu Fainali ya michuano hiyo inayoendelea nchini Ethiopia, baada ya kushinda michezo miwili ya awali ya Kundi B.
Simba Queens imemaliza ikiwa pointi saba huku Kawempe Muslim Ladies ya Uganda iliyoshika nafasi ya pili ikiwa na Pointi 6.
Katika mchezo wa Nusu Fainali, Simba Queens itacheza na Kenya Police Bullets, huku Kawempe Muslim Ladies ikikutana na wenyeji CBE ya Ethiopia.
Bingwa wa michuano hiyo atafuzu Kucheza Klabu Bingwa Afrika 2024/2025.
Tags: Simba Queens vs Kenya Police Bullets Nusu Fainali CECAFA