INEC Yasogeza Mbele Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura 2024
INEC Yasogeza Mbele Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura 2024
INEC Yasogeza Mbele Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura 2024, Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imetangaza kusogezwa mbele kwa zoezi la uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura hadi tarehe 20 Julai, 2024 badala ya tarehe 01 Julai, 2024 iliyopangwa hapo awali.
Akizungumza na waandishi wa habari mkoani Kigoma leo tarehe 22 Julai, 2024, Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji (Rufaa) Jacobs Mwambegele amesema kwamba uzinduzi wa zoezi hilo utafanyika siku ya Jumamosi tarehe 20 Julai, 2024 mkoani Kigoma ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (MB).
Mhe. Mwambegele ameeleza kwamba uamuzi huo wa Tume umetokana na kuzingatiwa kwa maoni ya wadau walioyatoa wakati wa mikutano iliyofanyika Jijini Dar es Salaam na Mkoani Kigoma.
“Tume imezingatia maoni na ushauri wa wadau. Hivyo, zoezi la uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura litaanza tarehe 20 hadi 26 Julai, 2024 badala ya tarehe 01 hadi 07 Julai, 2024, mkoani Kigoma na uzinduzi utafanyika siku hiyo ya tarehe 20 Julai, 2024 mkoani Kigoma ambapo Mgeni Rasmi atakuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb),” amesema.
Akizungumzia maoni hayo ya wadau, Mhe. Mwambegele amesema Tume imefanya mikutano tisa ya wadau ngazi ya Taifa mkoani Dar es Salaam kati ya tarehe 07 hadi 15 Juni, 2024 na mkutano mmoja wa wadau ngazi ya mkoa kwa mkoa wa Kigoma uliofanyika tarehe 19 Juni 2024.
Amewataja wadau waliokutana na Tume kuwa ni pamoja na Viongozi wa Vyama vya Siasa, Viongozi wa Dini, Wawakilishi wa Asasi za Kiraia, Wahariri wa Vyombo vya habari, Waandishi wa habari, Maafisa Habari wa Mikoa na Halmashauri, Wawakilishi wa Makundi mbalimbali ya Vijana, Watu wenye ulemavu, wanawake na Wazee wa Kimila.
Tags: 2024 badala ya tarehe 01 Julai, 2024 iliyopangwa hapo awali., INEC Yasogeza Mbele Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura 2024, Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imetangaza kusogezwa mbele kwa zoezi la uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura hadi tarehe 20 Julai
Je taarifa hii ni ya kweli?. Kusogezwa mbele Kwa uboreshaj wa daftari la kudumu la wapga kura