RATIBA YA LIGI KUU YA NBC 2024/2025 TAZAMA HAPA


INEC RATIBA YA UBORESHAJI WAPIGA KURA 2024/2025 HAPA


INEC KUITWA KWENYE USAILI 2024/2025 TAZAMA HAPA


AJIRA MPYA KILA SIKU TAFADHALI BONYEZA HAPA


JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP HAPA


NAFASI 20 za Watendaji wa Vijiji Kutoka Wilaya ya Shinyanga July 04-2024

Filed in Ajira by on 05/07/2024

NAFASI 20 za Watendaji wa Vijiji Kutoka Wilaya ya Shinyanga July 04-2024

NAFASI 20 za Watendaji wa Vijiji Kutoka Wilaya ya Shinyanga July 04-2024, NAFASI 20 za Watendaji Kutoka Wilaya ya Shinyanga July 04-2024, Nafasi 20 za Watendaji wa Vijiji Kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga July 04-2024, Nafasi za Kazi za Watendaji wa Vijiji Kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga 04-07-2024.

NAFASI 20 za Watendaji wa Vijiji Kutoka Wilaya ya Shinyanga July 04-2024

NAFASI 20 za Watendaji wa Vijiji Kutoka Wilaya ya Shinyanga July 04-2024, NAFASI 20 za Watendaji Kutoka Wilaya ya Shinyanga July 04-2024, Nafasi 20 za Watendaji wa Vijiji Kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga July 04-2024, Nafasi za Kazi za Watendaji wa Vijiji Kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga 04-07-2024.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga amepokea Kibali cha Ajira Mpya kutoka kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kupitia Barua yenye Kumb.Na.FA.97/228/01/09 ya tarehe 25.06.2024.

Hivyo, anakaribisha maombi ya kazi kutoka kwa Watanzania wenye sifa za kujaza nafasi zifuatazo:

✅MTENDAJI WA KIJIJI DARAJA LA III – NAFASI ISHIRINI (20)

SIFA ZA KUAJIRIWA.
Waombaji wanatakiwa wawe wenye Elimu ya Kidato cha Nne (Form IV) au Sita (Form Six) aliyehitimu astashahada/cheti katika moja ya fani zifuatazo: Utawala, Sheria, Elimu
ya Jamii, Usimamizi wa Fedha, Maendeleo ya Jamii na sayansi ya Sanaa kutoka Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo au Chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.

KAZI NA MAJUKUMU YA MTENDAJI WA KIJIJI DARAJA LA III

  • Afisa Masuuli na Mtendaji mkuu wa serikali ya Kijiji;
  • Kusimamia ulinzi na usalama wa raia na mali zao, kuwa mlinzi wa amani na msimamizi wa utawala bora katika Kijiji;
  • Kuratibu na kusimamia upangaji wa mipango ya maendeleo ya Kijiji;
  • Katibu wa mikutano na kamati zote za Halmashauri ya kijiji;
  • Katibu wa mikutano na kamati zote za Halmashauri ya kijiji;
  • Kutafsiri na Kusimamia Sera, Sheria na Taratibu;
  • Kuandaa taarifa ya utekelezaji wa kazi katika eneo lake na kuhamasisha wananchi katika kuandaa na kutekeleza mikakati ya kuondoa njaa, umaskini na
    kuongeza uzalishaji mali;
  • Kiongozi wa wakuu wa vitengo vya kitaalam katika kijiji;
  • Kusimamia, kukusanya na kuhifadhi kumbukumbu zote na nyaraka za kijiji;
  • Mwenyekiti wa kikao cha wataalam waliopo katika kijiji;
  • Kupokea, kusikiliza na kutatua malalamiko na migogoro ya wananchi;
  • Kusimamia utungaji wa Sheria Ndogo za kijiji; na
  • Atawajibika kwa Mtendaji Mkuu wa Kata.
  • Pamoja na kazi nyingine utakazopangiwa na Mwajiri wake.

MSHAHARA: Kwa kuzingatia ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS B

MASHARTI YA JUMLA

  • Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri wa kuanzia miaka18 na usiozidi miaka 45 isipokuwa kwa wale tu walioko kazini Serikalini;
  • Waombaji wawasilishe maelezo binafsi (Curriculum Vitae) yanayojitosheleza (Detailed CV) yenye Anuani na Namba za simu za kuaminika pamoja na majina
    ya wadhamini watatu (Referees) wa kuaminika.
  • Waombaji waambatanishe nakala za vyeti vya Kidato cha Nne au Sita, Taaluma na cheti cha kuzaliwa. Waombaji watakaowasilisha” Result Slip”,” Statement of
    Results”,” Provisional Results” au” Transcripts HAVITAKUBALIKA.
  • Kwa Waombaji waliosoma nje ya Nchi, Elimu ya Kidato cha Nne au Sita wawasilishe uthibitisho kutoka Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA).
  • Kwa waombaji waliosoma Vyuo nje ya Nchi wawasilishe uthibitisho kutoka Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU).
  • Waombaji watakokidhi sifa zinazotakiwa ndio watakaoitwa katika usaili.
  • Barua ya maombi iliyosainiwa na Mwombaji inaweza kuandikwa kwa lugha ya Kiingereza au Kiswahili.
  • Waombaji wenye mahitaji maalum (special needs/disability) wanatakiwa kuainisha kwenye maombi yao.
  • Waombaji watakaowasilisha Taarifa za kughushi watachukuliwa hatua kwa mujibu wa Sheria za Nchi.
  • Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali kutoka kwa Katibu Mkuu Kiongozi.

Mwisho wa kuwasilisha maombi ni tarehe 18 Julai, 2024.Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment
Portal) kupitia anuani ifuatayo; https://portal.ajira.go.tz (Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sektretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa ‘Recruitment Portal’).

Maombi yatakayowasiIishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo hili HAYATAFIKIRIWA.

Tags: , , , ,

Comments are closed.