NAFASI za Mwandishi Mwendesha Ofisi Kutoka Wilaya ya Shinyanga July 04-2024
NAFASI za Mwandishi Mwendesha Ofisi Kutoka Wilaya ya Shinyanga July 04-2024
NAFASI za Mwandishi Mwendesha Ofisi Kutoka Wilaya ya Shinyanga July 04-2024, Nafasi za Kazi za Mwandishi Mwendesha Ofisi Daraja La II Kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga July 04-2024, Ajira za Mwandishi Mwendesha Ofisi Daraja La II Kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga July 04-2024.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga amepokea Kibali cha Ajira Mpya kutoka kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kupitia Barua yenye Kumb.Na.FA.97/228/01/09 ya tarehe 25.06.2024.
Hivyo, anakaribisha maombi ya kazi kutoka kwa Watanzania wenye sifa za kujaza nafasi zifuatazo:
✅MWANDISHI MWENDESHA OFISI II (NAFASI 02)
SIFA ZA KUAJIRIWA.
Awe amefaulu Kidato cha Nne (IV) au kidato cha Sita (VI) wenye Stashahada (Diploma) ya Uhazili au Cheti cha NTA level 6 ya Uhazili.
Aidha awe amefaulu somo la Hatimkato ya Kiswahili na Kiingereza maneno 100 kwa dakika moja na kupata programu za compyuta za ofisi kama vile:- Word, Excel, Power point, Internet, E-mail na Publisher kutoka chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.
KAZI NA MAJUKUMU YA MWANDISHI MWENDESHA OFISI DARAJA LA II
- Kuchapa barua, taarifa na nyaraka za kawaida na za Siri;
- Kupokea wageni na kuwasaili shida zao na kuwaeleza wanapoweza kusaidiwa;
- Kutunza taarifa za kumbukumbu ya matuokio, miadi, tarehe za vikao, safari za Mkuu wake na ratiba za kazi zingine;
- Kutafuta majalada na nyaraka zinazohitajika katika utekelezaji wajukumu ya kazi;
- Kupokea majalada na kusambaza kwa maofisa walio katika
Divisheni/Kitengo/Sehemu husika; - Kukusanya, kutunza na kuyarejesha majalada na nyaraka sehemu zinahusika;
- Kupanga dondoo na kufanya maandalizi ya vikao mbalimbali;
- Kuandaa orodha ya mahitaji ya vifaa vya Ofisi.
MSHAHARA: Kwa kuzingatia ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS C
MASHARTI YA JUMLA
- Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri wa kuanzia miaka18 na usiozidi miaka 45 isipokuwa kwa wale tu walioko kazini Serikalini;
- Waombaji wawasilishe maelezo binafsi (Curriculum Vitae) yanayojitosheleza (Detailed CV) yenye Anuani na Namba za simu za kuaminika pamoja na majina
ya wadhamini watatu (Referees) wa kuaminika. - Waombaji waambatanishe nakala za vyeti vya Kidato cha Nne au Sita, Taaluma na cheti cha kuzaliwa. Waombaji watakaowasilisha” Result Slip”,” Statement of
Results”,” Provisional Results” au” Transcripts HAVITAKUBALIKA. - Kwa Waombaji waliosoma nje ya Nchi, Elimu ya Kidato cha Nne au Sita wawasilishe uthibitisho kutoka Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA).
- Kwa waombaji waliosoma Vyuo nje ya Nchi wawasilishe uthibitisho kutoka Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU).
- Waombaji watakokidhi sifa zinazotakiwa ndio watakaoitwa katika usaili.
- Barua ya maombi iliyosainiwa na Mwombaji inaweza kuandikwa kwa lugha ya Kiingereza au Kiswahili.
- Waombaji wenye mahitaji maalum (special needs/disability) wanatakiwa kuainisha kwenye maombi yao.
- Waombaji watakaowasilisha Taarifa za kughushi watachukuliwa hatua kwa mujibu wa Sheria za Nchi.
- Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali kutoka kwa Katibu Mkuu Kiongozi.
Mwisho wa kuwasilisha maombi ni tarehe 18 Julai, 2024.Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment
Portal) kupitia anuani ifuatayo; https://portal.ajira.go.tz (Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sektretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa ‘Recruitment Portal’).
Maombi yatakayowasiIishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo hili HAYATAFIKIRIWA.
POST: MWANDISHI MWENDESHA OFISI DARAJA LA II – 2 POST Employer: Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga More Details |
2024-07-18 Login to Apply |
Tags: Ajira za Mwandishi Mwendesha Ofisi Daraja La II Kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga July 04-2024., Nafasi za Kazi za Mwandishi Mwendesha Ofisi Daraja La II Kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga July 04-2024, NAFASI za Mwandishi Mwendesha Ofisi Kutoka Wilaya ya Shinyanga July 04-2024