NAFASI 9 za Watendaji wa Vijiji Kutoka Wilaya ya Kishapu July 04-2024
NAFASI 9 za Watendaji wa Vijiji Kutoka Wilaya ya Kishapu July 04-2024
NAFASI 9 za Watendaji wa Vijiji Kutoka Wilaya ya Kishapu July 04-2024, Nafasi za Kazi za Watendaji wa Vijiji Kutoka Halmashauri Wilaya ya Kishapu Leo July 04-2024, Ajira za Watendaji wa Vijiji Kutoka Halmashauri Wilaya ya Kishapu 04-07-2024.
Kwa mujibu wa kibali cha ajira mbadala chenye Kumb. Na. FA.97/288/01/09 cha tarehe 25 Juni, 2024 kutoka Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu anawatangazia wananchi wote Raia wa Tanzania kuomba nafasi za Kazi zifuatazo:-
✅MTENDAJI WA KIJIJI DARAJA III – (NAFASI – 9)
SIFA ZA MWOMBAJI
Mwombaji awe mwenye Elimu ya Kidato cha Nne (Form IV) au Sita (Form Six)
aliyehitimu astashahada/cheti katika moja ya fani zifuatazo: Utawala, Sheria, Elimu ya Jamii, Usimamizi wa Fedha, Maendeleo ya Jamii na sayansi ya Sanaa kutoka Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo au Chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.
KAZI NA MAJUKUMU YA MTENDAJI WA KIJIJI
- Afisa Masuuli na Mtendaji Mkuu wa Serikali ya Kijiji;
- Kusimamia ulinzi na Usalama wa raia na mali zao, kuwa Mlinzi wa Amani na
- Msimamizi wa Utawala Bora katika Kijiji,
- Kuratibu na kusimamia upangaji wa utekelezaji wa Mipango ya Maendeleo ya Jamii.
- Katibu wa Mikutano na Kamati zote za Halmashauri ya Kijiji.
- Kutafsiri na kusimamia Sera, Sheria na Taratibu;
- Kuandaa taarifa za utekelezaji wa kazi katika eneo lake na kuhamasisha wananchi katika kuandaa na kutekeleza mikakati ya kuondoa njaa, umaskini
na kuongeza uzalisha mali; - Kiongozi wa Wakuu wa Vitengo vya kitaalam katika kijiji
- Kusimamia, kukusanya na kuhifadhi kumbukumbu zote na nyaraka za kijiji.
- Mwenyekiti wa Kikao cha Wataalamu waliopo katika kijiji
- Kupokea, kusikiliza na kutatua malalamiko na migogoro ya wananchi.
- Kusimamia utungaji wa sheria ndogo za kijiji na
- Atawajibika kwa Mtendaji wa Kata.
NGAZI YA MSHAHARA: Kwa kuzingatia ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS B
MASHARTI YA JUMLA
- Mwombaji awe Raia wa Tanzania ambaye ana umri si zaidi ya Miaka 45 na sio pungufu ya Miaka 18.
- Mwombaji aambatishe nakala ya Cheti cha kuzaliwa.
- Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anuani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya Wadhamini (referees) watatu wa kuaminika pamoja na namba zao za Simu.
- Maombi yote yaambatane na nakala za vyeti vya Elimu na taaluma kutoka Vyuo vinavyotambuliwa na Serikali, na vilivyothibitishwa na Wakili au
Kamishna wa Viapo. - Testimonials, provision results, statement of results, havitakubaliwa
- Waombaji wote ambao wamesoma nje ya Nchi wahakikishe vyeti vyao
vinafanyiwa ulinganishi na TCU na NACTE. - Waomabji waambatanishe picha moja passport size ya hivi karibuni
- Barua ya Maombi iandikwe kwa Kiswahili au Kingereza
Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 17 Julai, 2024.
MUHIMU: Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa
pamoja na vyeti, aidha anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa;
Mkurugenzi Mtendaji,
Halmashauri ya Wilaya,
S.L.P 1288,
KISHAPU.
Maombi yote ya kazi yatumwe kwenye Mfumo wa Kieletroniki wa Ajira
(Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo: https://portal.ajira.go.tz/ anuani
hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Secretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu
iliyoandikwa “Recruitment Portal”
Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioanishwa katika tangazo hili
HAYATAFIKIRIWA.
POST: MTENDAJI WA KIJIJI III – 9 POST Employer: Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu More Details |
2024-07-17 Login to Apply |
Tags: Ajira za Watendaji wa Vijiji Kutoka Halmashauri Wilaya ya Kishapu 04-07-2024., NAFASI 9 za Watendaji wa Vijiji Kutoka Wilaya ya Kishapu July 04-2024, Nafasi za Kazi za Watendaji wa Vijiji Kutoka Halmashauri Wilaya ya Kishapu Leo July 04-2024