RATIBA YA LIGI KUU YA NBC 2024/2025 TAZAMA HAPA


INEC RATIBA YA UBORESHAJI WAPIGA KURA 2024/2025 HAPA


INEC KUITWA KWENYE USAILI 2024/2025 TAZAMA HAPA


AJIRA MPYA KILA SIKU TAFADHALI BONYEZA HAPA


JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP HAPA


NAFASI za Msaidizi Wa Kumbukumbu Halmashauri ya Mji wa Geita July 05-2024

Filed in Ajira by on 05/07/2024

NAFASI za Msaidizi Wa Kumbukumbu Halmashauri ya Mji wa Geita July 05-2024

NAFASI za Msaidizi Wa Kumbukumbu Halmashauri ya Mji wa Geita July 05-2024,Ajira za Msaidizi Wa Kumbukumbu Daraja II Kutoka Halmashauri ya Mji wa Geita Leo July 05-2024, Nafasi za Kazi za Msaidizi Wa Kumbukumbu Halmashauri ya Mji wa Geita tarehe 05-07-2024.

NAFASI za Msaidizi Wa Kumbukumbu Halmashauri ya Mji wa Geita July 05-2024

NAFASI za Msaidizi Wa Kumbukumbu Halmashauri ya Mji wa Geita July 05-2024,Ajira za Msaidizi Wa Kumbukumbu Daraja II Kutoka Halmashauri ya Mji wa Geita Leo July 05-2024, Nafasi za Kazi za Msaidizi Wa Kumbukumbu Halmashauri ya Mji wa Geita tarehe 05-07-2024.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Geita amepokea kibali cha Ajira mpya
kutoka kwa Katibu Mkuu OR – Utumishi chenye Kumb. Na. FA.97/288/01/09
cha terehe 25/06/2024.

Hivyo anapenda kuwatangazi watanzania wote wenye
sifa kutuma maombi kwa nafasi za Msaidizi wa Kumbukumbu II kama zilivyoainishwa kwa kuzingatia sifa tajwa:-

✅MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU II (“Records Management Assistant II”NAFASI 1)

SIFA ZA MWOMBAJI
Awe na Elimu ya kidato cha Nne (Form IV) au cha Sita (Form VI) aliehitimu
mafunzo ya stashahada/Diploma (NTA Level 6) katika fani ya Masijala kutoka
vyuo vinavyotambuliwa na Serikali, wenye ujuzi wa kompyuta.

KAZI NA MAJUKUMU YA MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU II.

  • Kutafuta kumbukumbu /nyaraka/mafaili yanayohitajika na wasomaji.
  • Kudhibiti upokeaji, uandikishaji wa Kumbukumbu/nyaraka.
  • Kuchambua, kuorodhesha na kupanga kumbukumbu/nyaraka katika makundi kulingana na somo husika (Classification and Boxing) kwa ajili ya matumizi ya ofisi.
  • Kuweka/kupanga kumbukumbu/nyaraka katika reki (File Racks/Cabinets) katika
    masjala/vyumba vya kuhifadhia kumbukumbu.
  • Kuweka kumbukumbu (barua, nyaraka nk) katika mafaili.
  • Kushughulikia maombi ya Kumbukumbu/Nyaraka kutoka Taasisi za Serikali.
  • Kutekeleza kazi zozote atakazokuwa amepangiwa na Msimamizi wake wa kazi.

NGAZI YA MSHAHARA: Kwa kuzingatia Ngazi za Mishahara ya Serikali- TGS C1

MASHARTI YA JUMLA KWA WAOMBAJI

  • Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania wenye umri wa miaka 18 nausiozidi miaka 45 isipo kuwa kwa wale tu walioko kazini Serikalini.
  • Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa kuainisha kwenye mfumo wa kuombea ajira Ulemavuwalionao kwa ajili ya taarifa kwa Sekretarieti ya ajira katika Utumishi wa Umma.
  • Waombaji waambatanishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anuani inayotumika, namba za simu zinazopatikana na anuani ya barua pepe (E-mail Adress) pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa
    kuaminika.
  • Waombaji ambao tayari ni watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia
    katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za kazi kwa waajiri wao na Waajiri wajiridhishe ipasavyo.
  • Maombi yote yaambatane na vyeti vya elimu na taaluma vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya Kidato cha Nne au Kidato cha Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa
    kuzingatia sifa za kazi husika
    Postgraduate/Degree/Advanced
    Diploma/Diploma/Certificate – Cheti cha Mtihani wa Kidato cha nne na
    cha Sita, Computer Certificate, – Vyeti vya Kitaaluma (Proffessional
    Certificate from Respective Boards).
  • Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati za matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
  • Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na Vimethibitishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTVET).
  • Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
  • Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa Umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo
    katika Waraka Na. CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010.
  • Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
  • Waombaji watakaowasilisha taarifa na sifa za kughushi watachukuliwa hatua za kisheria.

Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 17 Julai, 2024.

MUHIMU: kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliosainiwa
pamoja na vyeti vya elimu. anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa:-
Mkurugenzi,
Halmashauri Ya Mji Geita,
S.L.P 384,
GEITA.

Maombi yote ya kazi yatumwe kwenye mfumo wa kielekroniki wa
ajira(Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo https://portal.ajira.go.tz/ (Anuani
hii pia inapaikana kwenye Tovuti ya Sekretariet ya Ajira kwa kuingia sehemu
iliyoandikwa ‘Recruitment Portal’).

Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulio ainishwa katika tangazo hili HAYATAFIKIRIWA.

Tags: , ,

Comments are closed.