NAFASI za Mwandishi Mwendesha Ofisi Halmashauri ya Mji wa Geita July 05-2024
NAFASI za Mwandishi Mwendesha Ofisi Halmashauri ya Mji wa Geita July 05-2024
NAFASI za Mwandishi Mwendesha Ofisi Halmashauri ya Mji wa Geita July 05-2024, Nafasi za Kazi za Mwandishi Mwendesha Ofisi Kutoka Halmashauri ya Mji wa Geita July 05-2024, Nafasi za Kazi za Mwandishi Mwendesha Ofisi Daraja II kutoka Halmashauri ya Mji wa Geita Leo July 05-2024.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Geita amepokea kibali cha Ajira mpya
kutoka kwa Katibu Mkuu OR – Utumishi chenye Kumb. Na. FA.97/288/01/09
cha terehe 25/06/2024.
Hivyo anapenda kuwatangazi watanzania wote wenye
sifa kutuma maombi kwa nafasi za Mwandishi Mwendesha ofisi II kama zilivyoainishwa kwa kuzingatia sifa tajwa:-
✅MWANDISHI MWENDESHA OFISI II (“Office Management Secretary
II”NAFASI 1)
SIFA ZA MWOMBAJI
Awe amehitimu Elimu ya Kidato cha Nne (Form IV) au cha Sita (Form VI), aliyefuzu
mafunzo ya Stashahada ya uhazili (NTA LEVEL 6), Awe amefaulu somo la
Hatimkato ya Kiswahili na Kiingereza maneno 100 kwa dakika moja.
Awe amepata mafunzo ya Komputa kutoka chuo chochote kinachotambulika na Serikali na kupata cheti katika “Program za Windows, Microsoft Office, Internet, E-mail na Publisher”.
KAZI NA MAJUKUMU YA MWANDISHI MWENDESHA OFISI II.
- Kuchapa barua, taarifa na nyaraka za kawaida.
- Kusaidia kupokea wageni na kuwasaili shida zao na kuwaelekeza sehemu wanapoweza kushughulikiwa.
- Kusaidia kutunza taarifa/ Kumbukumbu za matukio, miadi, wageni, tarehe za vikao, safari za Mkuu wake na ratiba ya kazi zingine zilizopangwa kutekelezwa
katika Ofisi anayofanyia kazi, kumuarifu Mkuu wake kwa wakati unaohitajika. - Kusaidia kutafuta na kumpatia Mkuu wake majalada, nyaraka au kitu chochote kinachohitajika katika shughuli za kazi hapo ofisini.
- Kusaidia kufikisha maelekezo ya Mkuu wake wa kazi kwa wasidizi wake na pia kumuarifu kuhusu taarifa zozote anazokuwa amepewa na wasaidizi hao.
- Kusaidia kupokea majalada, kugawa kwa maofisa walio katika sehemu alipo na kuyakusanya, kuyatunza na kuyarudisha sehemu zinazohusika.
- Kutekeleza kazi zozote atakazokuwa amepangiwa na Msimamizi wake wa kazi.
NGAZI YA MSHAHARA: Kwa kuzingatia Ngazi za Mishahara ya Serikali- TGS C1
MASHARTI YA JUMLA KWA WAOMBAJI
- Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania wenye umri wa miaka 18 nausiozidi miaka 45 isipo kuwa kwa wale tu walioko kazini Serikalini.
- Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa kuainisha kwenye mfumo wa kuombea ajira Ulemavuwalionao kwa ajili ya taarifa kwa Sekretarieti ya ajira katika Utumishi wa Umma.
- Waombaji waambatanishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anuani inayotumika, namba za simu zinazopatikana na anuani ya barua pepe (E-mail Adress) pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa
kuaminika. - Waombaji ambao tayari ni watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia
katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za kazi kwa waajiri wao na Waajiri wajiridhishe ipasavyo. - Maombi yote yaambatane na vyeti vya elimu na taaluma vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya Kidato cha Nne au Kidato cha Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa
kuzingatia sifa za kazi husika
Postgraduate/Degree/Advanced
Diploma/Diploma/Certificate – Cheti cha Mtihani wa Kidato cha nne na
cha Sita, Computer Certificate, – Vyeti vya Kitaaluma (Proffessional
Certificate from Respective Boards). - Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati za matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
- Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na Vimethibitishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTVET).
- Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
- Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa Umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo
katika Waraka Na. CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010. - Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
- Waombaji watakaowasilisha taarifa na sifa za kughushi watachukuliwa hatua za kisheria.
Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 17 Julai, 2024.
MUHIMU: kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliosainiwa
pamoja na vyeti vya elimu. anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa:-
Mkurugenzi,
Halmashauri Ya Mji Geita,
S.L.P 384,
GEITA.
Maombi yote ya kazi yatumwe kwenye mfumo wa kielekroniki wa
ajira(Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo https://portal.ajira.go.tz/ (Anuani
hii pia inapaikana kwenye Tovuti ya Sekretariet ya Ajira kwa kuingia sehemu
iliyoandikwa ‘Recruitment Portal’).
Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulio ainishwa katika tangazo hili HAYATAFIKIRIWA.
POST: MWANDISHI MWENDESHA OFISI DARAJA LA II – 1 POST Employer: Halmashauri ya Mji wa Geita More Details |
2024-07-18 Login to Apply |
Tags: Nafasi za Kazi za Mwandishi Mwendesha Ofisi Daraja II kutoka Halmashauri ya Mji wa Geita Leo July 05-2024., Nafasi za Kazi za Mwandishi Mwendesha Ofisi Kutoka Halmashauri ya Mji wa Geita July 05-2024, NAFASI za Mwandishi Mwendesha Ofisi Halmashauri ya Mji wa Geita July 05-2024