CRESCENTIUS Magori Azungumzia Sakata la Usajili wa Lameck Lawi
CRESCENTIUS Magori Azungumzia Sakata la Usajili wa Lameck Lawi
CRESCENTIUS Magori Azungumzia Sakata la Usajili wa Lameck Lawi, Mjumbe wa Bodi ya Klabu ya Simba, Crescentius Magori amesema kuwa Sakata la mchezaji Lameck Lawi litaamuliwa na mamlaka zinazosimamia Mpira wa Miguu nchini kwani wamekwisha liwasilisha.
Magori amesisitiza kuwa Lawi ni mchezaji halali wa Simba kwa sababu walifuata taratibu zote katika kukamilisha usajili wake kwa kuilipa Costal Union fedha yote waliyokubaliana pamoja na kumlipa mchezaji
“Jambo la Lameck Lawi limezuka tatizo sisi tumemsajili, tukalipa fedha kwa timu na tukamlipa pia mchezaji mwenyewe lakini yakatokea yaliyotoea na suala hilo limeshafika kwenye mamlaka husika”
“Coastal ni ndugu zetu ninaamini jambo hilo litaisha halipaswi kuchukua muda mrefu, msimamo wa Simba ni kwamba mchezaji tumemsajili kwasababu alikuwa kwenye mipango yetu, na hakuna haja ya kurushiana maneno mamlaka zitasema ukweli, ” alisema Magori
Lawi hakuungana na kikosi cha Simba kilichoweka kambi Misri kwa ajili ya pre-season beki huyo akiendelea kusalia katika klabu ya Coastal Union
Kuna taarifa kuwa Coastal Union wamepokea ofa nono zaidi kutoka timu nyingine ya nje ya nchi na wamekusudia kumuuza tena beki huyo
Hata hivyo walipokea ofa hiyo wakiwa tayari wameshafanya biashara na Simba.
Katika hatua nyingine, Crescentus Magori amesema kuwa licha ya maboresho makubwa yaliyofanyika mpaka sasa, bado hawajafunga zoezi la usajili.
Aidha Magori alithibitisha kuwa Simba huenda ikaachana na wachezaji zaidi akiwemo winga, Aubin Kramo ambaye uongozi unaendelea kuzungumza nae kuhusu mustakabali wake
“Tumefanya usajili mkubwa mpaka sasa lakini nisema tu, bado hatujafunga usajili”
“Kramo hajacheza kwa muda mrefu sana kutokana na majeraha, huenda tukamtoa kwa mkopo au tukamuacha,” alisema Magori
Magori aliweka bayana malengo ya Simba kuelekea msimu ujao wa 2024/2025 kuwa ni kushinda mataji ya ndani pamoja na kutwaa Ubingwa wa kombe la Shirikisho la CAF (CAF Confederation Cup)
Tags: CRESCENTIUS Magori Azungumzia Sakata la Usajili wa Lameck Lawi